Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Hispania

Manuel Azana, rais wa Jamhuri ya Hispania

Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Hispania ilipiganiwa miaka ya 1936-1939 kati ya watetezi wa serikali ya Jamhuri ya Hispania na wafuasi wa kiongozi wa kijeshi jenerali Francisco Franco.

Hatimaye Franco alishinda akawa kiongozi na dikteta wa Hispania hadi kifo chake mwaka 1975.

Utangulizi wa vita

Siasa ya Hispania ilikuwa katika hali ya vurugu tangu kuanzishwa kwa jamhuri ya pili mwaka 1931 iliyomaliza utawala wa mfalme Alfonso XIII. Sehemu kubwa za wafanyakazi wa viwandani hazikuridhika na jamhuri, wakalenga mapinduzi ya kijamii.

Harakati kali ya upinzani dhidi ya nafasi kubwa ya Kanisa Katoliki katika taifa la Hispania ilisababisha mashambulio shidi ya makanisa na monasteri na kifodini cha Wakristo wengi, hasa mapadri na watawa.

Wafuasi wa mfalme aliyeondoka nchini, watetezi wa Kanisa Katoliki, wenye mashamba makubwa na chama kipya cha Falange walianza kuungana kupinga kwa jamhuri na katiba yake kwa jumla.

Baada ya majaribio ya vikosi vya wafanyakazi wasoshalisti, lakini pia wanajeshi wapenzi wa mfalme waliolenga wote kupindua serikali, uchaguzi wa 1936 haukuleta usuluhisho wa matata ya siasa. Vikundi viwili vikubwa vilivyoshindana vilikuwa "umoja wa wananchi" uliounganisha wasoshalisti, wakomunisti na vikundi vidogo dhidi ya "umoja wa taifa" uliounganisha wafuasi wa mfalme, Wakatoliki, chama cha wenye mashamba na Falange. Umoja wa wananchi ulipata kura chache zaidi kuliko wapinzani wake na sheria ya uchaguzi uliupa nafasi nyingi bungeni.

Other Languages
беларуская (тарашкевіца)‎: Грамадзянская вайна ў Гішпаніі
brezhoneg: Brezel Spagn
français: Guerre d'Espagne
Fiji Hindi: Spanish Civil War
Bahasa Indonesia: Perang Saudara Spanyol
한국어: 스페인 내전
Lëtzebuergesch: Spuenesche Biergerkrich
Plattdüütsch: Spaansche Börgerkrieg
नेपाल भाषा: स्पेनी गृहयुद्ध
srpskohrvatski / српскохрватски: Španski građanski rat
Simple English: Spanish Civil War
Bân-lâm-gú: Se-pan-gâ Lōe-chiàn