Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia

Shirikiano za kijeshi katika Ulaya mwaka 1915. Nyekundu: Mataifa ya Kati; kijani: Mataifa ya Ushirikiano; njano: mataifa yasiyoshiriki vita
Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia: <br />1.Mifereji huko Verdun (Ufaransa) baada ya kulimwa kwa mizinga mikubwa; <br />2. Ndege za kijeshi na faru za kwanza; <br />3. bunduki ya mtombo na manowari
Ramani ya dunia ikionyesha nchi na maeneo yaliyoshiriki katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Kijani: Mataifa ya Ushirikiano; njano: Mataifa ya Kati ; nchi zisizoshiriki kwa rangi ya kijivu

Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilikuwa vita iliyopigwa kuanzia mwaka 1914 hadi 1918. Mataifa wapiganaji yalikuwa Ujerumani, Austria-Hungaria, Bulgaria na Uturuki (ziliitwa "Mataifa ya Kati", ing. central powers) kwa upande mmoja dhidi ya Ufaransa, Urusi, Uingereza, Italia, Marekani na nchi mbalimbali zilizoshirikiana nazo (zilitwa "Mataifa ya Ushirikiano", ing. allied powers).

Vita hii ilianza katika Ulaya ikapanuka haraka hadi Mashariki ya Kati, Afrika na Asia ya Mashariki ikasababisha kifo cha takriban watu milioni tisa.

Sababu na matokeo

Sababu yake ilikuwa mashindano makali kati ya mataifa ya Ulaya kuhusu kushika nafasi ya kipaumbele barani Ulaya na duniani kote.

Matokeo yake yalikuwa mwisho wa kipaumbele cha Ulaya duniani na kupanda ngazi kwa Marekani, mapinduzi katika nchi mbalimbali, mwisho wa falme za Ujerumani, Austria na Urusi pamoja na mwanzo wa utawala wa kikomunisti katika Urusi, mwisho wa Dola la Austria-Hungaria na wa Dola la Uturuki la Kiosmani pamoja na mwisho wa ukoloni wa Kijerumani duniani.

Katika Ulaya nchi mpya zilijitokeza kama vile Chekoslovakia, Ufini, Latvia, Estonia na Yugoslavia pamoja na nchi za zamani zilizotokea tena katika uwanja wa kimataifa ndizo Austria, Hungaria, Lithuania na Poland.

Other Languages
Alemannisch: Erster Weltkrieg
žemaitėška: Pėrma svieta vaina
беларуская (тарашкевіца)‎: Першая сусьветная вайна
qırımtatarca: Birinci Cian cenki
emiliàn e rumagnòl: Prémma guèra mundièl
English: World War I
Esperanto: Unua mondmilito
estremeñu: I Guerra Mundial
Nordfriisk: Iarst Wäältkrich
Gàidhlig: An Cogadh Mòr
客家語/Hak-kâ-ngî: Thi-yit-chhṳ Sṳ-kie Thai-chan
Fiji Hindi: World War I
Bahasa Indonesia: Perang Dunia I
Patois: Wol Waar I
Basa Jawa: Perang Donya I
къарачай-малкъар: Биринчи дуния къазауат
Lëtzebuergesch: Éischte Weltkrich
Bahasa Melayu: Perang Dunia Pertama
မြန်မာဘာသာ: ပထမ ကမ္ဘာစစ်
مازِرونی: جهونی جنگ اول
Dorerin Naoero: Eaket Eb I
Plattdüütsch: Eerste Weltkrieg
Nedersaksies: Eerste Wealdkrieg
नेपाल भाषा: तःहताः १
norsk nynorsk: Den fyrste verdskrigen
srpskohrvatski / српскохрватски: Prvi svjetski rat
Simple English: World War I
slovenščina: Prva svetovna vojna
Soomaaliga: Dagaalkii koowaad
српски / srpski: Први светски рат
Basa Sunda: Perang Dunya I
Türkmençe: Birinji jahan urşy
ئۇيغۇرچە / Uyghurche: بىرىنچى دۇنيا ئۇرۇشى
oʻzbekcha/ўзбекча: Birinchi jahon urushi
vepsän kel’: Ezmäine mail'man voin
Volapük: Volakrig balid