Visiwa vya South Georgia na South Sandwich

Mahali pa South Georgia
na South Sandwich katika Atlantiki Kusini
Ramani ya visiwa
Makazi ya zamani kwenye kisiwa cha South Georgia pamoja na kijiji hai cha Grytviken
Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Visiwa vya South Georgia na South Sandwich ni eneo la ng'ambo la Uingereza kusini mwa Bahari Atlantiki.

Eneo hilo ni mafunguvisiwa mawili ya South Georgia na Sandwich, halafu visiwa vingine vidogo sana vilivyosambaa katika maeneo mapana ya Atlantiki Kusini.

Visiwa vyote vina eneo la km² 3,900.

Idadi ya wakazi ni 20 na wengi wao ni wanasayansi wanaochungulia ndege wanaokaa kwenye visiwa pamoja na afisa mmoja mwakilishi wa serikali ya Uingereza.

Wakazi

Hakuna wenyeji kwenye visiwa hivi. Tangu karne ya 19 wavuvi wa nyangumi kutoka Ulaya walijenga huk vituo ambako walipeleka nyangumi kwa kuwakatakata na kupika mafuta yao. Vituo hivyo vilikuwa na makumi hadi mamia ya wakazi wakati wa kuwinda nyangumi lakini wakati wa baridi ni watu wachache tu waliobaki. Vituo hivyo vilifungwa katika miaka ya 1960 kutokana na kupotea kwa nyangumi.

Mwaka 1904 mvuvi kutoka Norwei alianzisha kijiji cha Grytviken kama kituo cha kupikia mafuta ya nyangumi na kijiji hicho ni makazi pekee ya kudumu kwenye visiwa hivi hadi leo.

Other Languages
srpskohrvatski / српскохрватски: Južna Georgija i arhipelag Južni Sandwich