Uvuvi

Wavuvi katika bandari ya Kochi, India.

Uvuvi ni kazi ya kukamata samaki ndani ya maji na kuwaweka nje yake, lakini pia kufuga samaki na wanyama wengine wa majini.

Kusudi lake ni hasa kupata chakula (kitoweo) na muda mwingine hufanywa kama biashara ili kujipatia kipato. Tena siku hizi uvuvi unatokea pia kama burudani, katika utalii na kama sehemu ya michezo.

Uvuvi ni kati ya shughuli za kale kabisa za binadamu na katika uchumi huhesabiwa katika sekta za msingi pamoja na kilimo na uchimbaji wa madini. Kutokana na takwimu za FAO kuna watu milioni 38 duniani wanaofanya kazi ya kuvua au kufuga samaki na hivyo husaidia kukuza uchumi wa nchi fulani.

Pamoja na wengine wanaosafirisha windo na kulifanyia kazi viwandani au kuliuza masokoni, madukani au kwenye hoteli kuna zaidi ya watu milioni 500 wanaokimu maisha yao kutokana na sekta hii ya uvuvi. [1]

Uvuvi hufanywa penye magimba ya maji kama vile bahari, maziwa, mito au mabwawa. Mara nyingi wavuvi hutumia chombo cha kusafiria majini kama boti lakini wengine wanakaa ufukoni na kuvua kutoka nchi kavu.

Vyombo vya uvuvi ni aina za nyavu zinazoweza kushika samaki na kumvuta nje ya maji, ndoano au pia aina za mikuki inayolenga samaki walio karibu na uso wa maji.

Tunapaswa kulinda bahari, maziwa pamoja na mito ili mazalia ya samaki yazidi kuongezeka na pia tupige vita uvuvi haramu kwa kuwa husababisha kuwa nyuma kwa uvuvi.

Inabidi serikali ziweke ulinzi kwenye suala la uvuvi kwani kuna wavuvi haramu wanaotumia sumu, baruti na vinginevyo vingi ambavyo havitakiwi katika uvuvi.

Marejeo

  1. ftp://ftp.fao.org/FI/brochure/climate_change/policy_brief.pdf Fish (including shellfish) provides essential nutrition for 3 billion people and at least 50% of animal protein and minerals to 400 million people in the poorest countries. • Over 500 million people in developing countries depend, directly or indirectly, on fisheries and aquaculture for their livelihoods. • Aquaculture is the world’s fastest growing food production system, growing at 7% annually. • Fish products are among the most widely traded foods, with more than 37% by volume of world production traded internationally.
Other Languages
Afrikaans: Visvang
aragonés: Pesca
Ænglisc: Fiscoþ
العربية: صيد الأسماك
asturianu: Pesca
azərbaycanca: Balıqçılıq
تۆرکجه: بالیقچیلیق
български: Риболов
Bahasa Banjar: Maunjun
brezhoneg: Peskerezh
bosanski: Ribolov
català: Pesca
کوردی: ڕاوەماسی
čeština: Rybolov
Cymraeg: Pysgota
Ελληνικά: Αλιεία
English: Fishing
Esperanto: Fiŝkaptado
español: Pesca
eesti: Kalapüük
euskara: Arrantza
suomi: Kalastus
Gaeilge: Iascaireacht
Gàidhlig: Iasgach
galego: Pesca
Avañe'ẽ: Pirakutu
ગુજરાતી: માછીમારી
עברית: דיג
hrvatski: Ribolov
magyar: Halászat
Bahasa Indonesia: Penangkapan ikan
Ido: Peskado
íslenska: Fiskveiðar
日本語:
Basa Jawa: Mancing
Kabɩyɛ: Pɔɔ cɔlʋʋ
한국어: 어로
Latina: Piscatus
Lëtzebuergesch: Fëscherei
Limburgs: Vèsserij
lietuvių: Žūklė
latviešu: Zvejošana
македонски: Риболов
Nāhuatl: Michmāliztli
Napulitano: Pesca
Plattdüütsch: Fischeree
Nedersaksies: Visserieje
नेपाली: माछा पालन
Nederlands: Visserij
norsk nynorsk: Fiske
norsk: Fiske
Nouormand: Pêque
occitan: Pesca
Picard: Péqueu
português: Pesca
Runa Simi: Challwa hap'iy
română: Pescuit
русский: Рыбная ловля
Kinyarwanda: Uburobyi
саха тыла: Балыктааһын
sicilianu: Pisca
Scots: Fishin
srpskohrvatski / српскохрватски: Ribolov
Simple English: Fishing
slovenčina: Rybolov
slovenščina: Ribolov
српски / srpski: Риболов
svenska: Fiske
Türkçe: Balıkçılık
українська: Рибальство
oʻzbekcha/ўзбекча: Baliq ovlash
vepsän kel’: Kalatez
Tiếng Việt: Ngư nghiệp
walon: Pexhe
Winaray: Pangingisdâ
中文: 捕魚
粵語: 捉魚