Uvimbe wa sikio

Uvimbe wa sikio
Mwainisho na taarifa za nje
A bulging tympanic membrane with cloudy fluid behind it as is typical in a case of acute otitis media
ICD-1065.-67.
ICD-9017.40, 055.2, 381.0, 381.1, 381.2, 381.3, 381.4, 382
DiseasesDB29620 serous,
9406 suppurative
MedlinePlus000638 acute, Kigezo:MedlinePlus2 with effusion, Kigezo:MedlinePlus2 chronic
eMedicineemerg/351
ent/426 complications, ent/209 with effusion, ent/212 Medical treat., ent/211 Surgical treat. ped/1689
MeSHD010033

Uvimbe wa sikio ni kikundi cha magonjwa ya uvimbe wa sehemu ya katikati mwa sikio.[1] Aina mbili kuu ni uvimbe mkali wa sikio (AOM) na uvimbe wa sikio ulio na mchozo (OME).[2] AOM ni maambukizi yanayoanza ghafla yanayodhihirika kwa maumivu ya sikio. Katika watoto wadogo, maumivu haya yanaweza kupelekea kulia sana, na ugumu wa kulala. Decreased eating and a fever may also be present. OME is typically not associated with symptoms.[3] Mara kwa mara, mgonjwa huhisi kujaa sikioni. Ugonjwa huu hufasiliwa kama uwepo wa kiowevu kisichoambukiza cha Zaidi ya wiki mbili katika sehemu ya katikati mwa sikio kwa zaidi ya miezi mitatu. Uvimbe wa sikio wa muda mrefuunaotoa usaha (CSOM) ni uvimbe wa sehemu ya katikati mwa sikio wa zaidi ya wiki mbili unaosababisha vipindi vya kutokwa na usaha sikioni. Hali hii inaweza kuwa tatizo la uvimbe mkali wa sikio. Ni nadra usaha kuwepo.[4] Hali zote tatu zinaweza kuhusishwa na kuppoteza uwezo wa kusikia.[1][2] Kupoteza uwezo wa kusikia katika OME kunaweza kutatiza uwezo wa kusoma kwa mtoto, kwa sababu ya hali yake ya muda mrefu.[4]

Kisababishi na utambuzi

Kisababishi cha AOM kinahusiana na anatomia ya utotoni na utendakazi wa kingamwili. Bakteria au virusivinaweza kuhusishwa. Vipengele vya hatari vinahusisha: kuhatarishwa kwa moshi, utumiaji vitulizaji, na kutembelea vituo vya utunzaji. Hali hutokea mara nyingi katika watu ambao ni Wamarekani Asilia au walio na Dalili za Down.[4] OME mara nyingi hutokea kufuatia AOM lakini pia inaweza kuhusishwa na maambukizi ya sehemu ya juu ya njia ya pumzi yanayosababishwa na virusi, vitu vinavyowasha kama vile moshi, au mzio.[4][2] Kuchunguza kiwambo cha sikio ni hatua muhimu katika utambuzi sahihi.[5] Dalili za AOM ni pamoja nakuvimba au ukosefu wa mwendo wa utando wa kiwambo kutokana na kipenga cha hewa.[6][3] Mchozo mpya usiohusiana na uvimbe wa sehemu ya nje ya sikio pia ni dalili ya uwepo wa ugonjwa huu.[3]

Other Languages
Acèh: Tungkiëk
Aymar aru: Jinchu usu
български: Отит
English: Otitis media
español: Otitis media
Հայերեն: Ականջահոսք
Bahasa Indonesia: Radang telinga tengah
italiano: Otite media
日本語: 中耳炎
한국어: 중이염
português: Otite média
Runa Simi: Rinri nanay
română: Otită
русский: Средний отит
srpskohrvatski / српскохрватски: Zapaljenje srednjeg uva
Tiếng Việt: Viêm tai giữa
中文: 中耳炎