Utoaji mimba

Mimba ya wiki 10 hivi iliyotolewa tumboni mwa mama kwa njia ya upasuaji.

Utoaji mimba au Uavyaji wa mimba ni tendo la hiari la kuua mimba iliyokwishatungwa tumboni mwa mwanamke. Unaweza kufanywa naye au na watu wengine kwa kibali chake au bila ya hicho.

Sababu zinaweza kuwa mbalimbali: hatari kwa uhai wa mjamzito, haya kwa tendo lililotunga mimba kinyume cha maadili, hali ya uchumi, ulemavu wa mama au wa mimba, ubaguzi wa jinsia n.k.

Ni tofauti na tukio lisilokusudiwa la mimba kuharibika kwa sababu mbalimbali.

Mbinu zake

Mimba inaweza ikatolewa kwa hiari kwa njia nyingi. Namna iliyochaguliwa hutegemea hasa umri wa kiinitete au kijusi, ambacho hukua kwa ukubwa kadiri siku zinavyopita. [1]

Mbinu inaweza ikachaguliwa kulingana na uhalalisho wa utoaji mimba, upatikanaji, na uamuzi wa daktari na mjamzito.

Kwa kutumia dawa

Utoaji mimba ambao unatumia dawa huchangia 10% ya utoaji mimba wote huko Marekani na Ulaya.

Iwapo itashindikana kutoa mimba kwa njia hiyo, usafishaji wa ombwe au uondoaji kwa mikono hutumika.

Upasuaji

Katika wiki 12 za kwanza, ufyonzaji au kuavya kwa uvutaji ombwe ndiyo mbinu inayotumika sana.

Utanuaji na ukwanguaji ni njia ya pili inayotumiwa sana katika uavyaji mimba, ni utaratibu wa wastani wa kiginakolojia unaofanywa kwa sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa uvimbe wowote hatari katika ukuta wa mfuko wa uzazi, uchunguzi wa utokaji damu usiokuwa wa kawaida na utoaji wa mimba.

Mbinu nyingine lazima zitumike tu kuavya mimba katika miezi mitatu ya pili ya ujauzito. Uzazi wa kabla ya kipindi kuwadia unaweza kuchochewa kwa kutumia dawa zinazotoa mimba; hii inaweza kuambatanishwa na kudungwa sindano iliyo na mchanganyiko wa toni ya misuli (haipatoni) pamoja na chumvi au urea kwenye majimaji ya amnioni.

Baada ya wiki 16 za ujauzito, uavyaji mimba unaweza kusababishwa kwa utanuaji na uchopoaji kamili, yaani ugandamuaji wa fuvu la kichwa kizazini, ambao huhitaji ugandamuaji wa fuvu la kichwa cha kijusi kabla ya kuchopolewa. Wakati mwingine huitwa "uzazi mdogo wa utoaji mimba", ambao umepigwa marufuku nchini Marekani.

Utoaji mimba kwa njia ya histerotomia ni utaratibu sawa na upasuaji wa sehemu na unafanya kazi chini ya dawa ya usingizi wa ujumla. Huhitaji upasuaji mdogo ukilinganishwa na upasuaji mkubwa na hutumika ujauzito ukiwa kwenye hatua za mwisho.

Kutoka wiki ya 20 mpaka ya 23 ya umri wa mimba, sindano ya kuzuia moyo wa kichanga inaweza ikatumika kama awamu ya kwanza ya utoaji mimba kwa taratibu za kiupasuaji[2][3] [4] [5] [6] [7] na kuhakikisha kwamba kijusi si kizaliwa hai. [8]

Njia nyinginezo

Kihistoria, idadi ya mimea inayosadikika kuna na uwezo wa kutoa mimba zimetumika katika utabibu wa asili: tansia, penniroyali, kohoshi mweusi, na silifiamu iliyopo sasa. [9] Matumizi ya mitishamba kwa namna fulani yanaweza kusababisha hata madhara yaletayo kifo, kama vile kushindwa kwa viungo mbalimbali vya mwili, na hazipendekezwi na daktari. [10]

Utoaji mimba wakati mwingine ni kujaribu na kusababisha athari ya maumivu ya tumbo. Kiwango cha nguvu, kikiwa kikali, kinaweza kusababisha majeraha makubwa ndani bila ya ulazima wa mimba kutoka.

Katika Asia ya Kusini, kuna mapokeo ya kujaribu kutoa mimba kwa kuchua tumbo kwa nguvu. Moja ya mabango ya michoro ya mapambo ya hekalu la Angkor Wat katika Cambodia linaonyesha pepo likifanya utoaji mimba kwa mwanamke ambaye alimtuma kutoka kuzimu.

Mbinu nyingine iliyoripotiwa ya utoaji mimba wa kujitegemea ni pamoja na matumizi mabaya ya dawa inayofanana na vichocheo vya mwili yaani misoprostoli, na uingizaji wa vifaa visivyo vya kiupasuaji kama sindano za kufumia na kiango cha nguo ndani ya mji wa mimba.

Other Languages
Afrikaans: Aborsie
aragonés: Alborto
العربية: إجهاض
مصرى: اجهاض
asturianu: Albuertu
azərbaycanca: Abort
башҡортса: Аборт
žemaitėška: Abuorts
беларуская: Аборт
беларуская (тарашкевіца)‎: Аборт
български: Аборт
বাংলা: গর্ভপাত
bosanski: Pobačaj
català: Avortament
کوردی: لەبەرچوون
čeština: Interrupce
Cymraeg: Erthyliad
dansk: Abort
Zazaki: Kurtaj
Ελληνικά: Έκτρωση
English: Abortion
Esperanto: Aborto
español: Aborto
eesti: Abort
euskara: Abortu
فارسی: سقط جنین
suomi: Abortti
føroyskt: Fosturtøka
français: Avortement
Frysk: Abortus
Gaeilge: Ginmhilleadh
galego: Aborto
Avañe'ẽ: Membykua
हिन्दी: गर्भपात
Fiji Hindi: Abortion
hrvatski: Pobačaj
Հայերեն: Վիժում
interlingua: Aborto
Bahasa Indonesia: Gugur kandungan
Ilokano: Alis
íslenska: Fóstureyðing
italiano: Aborto
ᐃᓄᒃᑎᑐᑦ/inuktitut: ᐃᓄᐃᑎᑦᑐᖅ
日本語: 妊娠中絶
Patois: Abaashan
Basa Jawa: Aborsi
ქართული: აბორტი
Kabɩyɛ: Hɔɔ lɩzɩɣ
қазақша: Аборт
한국어: 낙태
Кыргызча: Аборт
Latina: Abortus
Lëtzebuergesch: Ofdreiwung
Limburgs: Abortus
lumbaart: Abort
lietuvių: Abortas
latviešu: Aborts
मैथिली: गर्भपतन
Malagasy: Fanalan-jaza
македонски: Абортус
മലയാളം: ഗർഭഛിദ്രം
монгол: Аборт
मराठी: गर्भपात
Bahasa Melayu: Pengguguran
Malti: Abort
नेपाली: गर्भपतन
Nederlands: Abortus
norsk nynorsk: Abort
norsk: Abort
Chi-Chewa: Kuchotsa mimba
occitan: Avortament
ଓଡ଼ିଆ: ଗର୍ଭପାତ
ਪੰਜਾਬੀ: ਗਰਭਪਾਤ
Kapampangan: Abortion
polski: Aborcja
Piemontèis: Abòrt
پنجابی: ابورشن
português: Aborto
Runa Simi: Sulluchiy
română: Avort
русский: Аборт
русиньскый: Аборт
srpskohrvatski / српскохрватски: Abortus
සිංහල: ගබ්සාව
Simple English: Abortion
slovenčina: Interrupcia
slovenščina: Splav
chiShona: Kubvisa nhumbu
српски / srpski: Побачај
svenska: Abort
తెలుగు: గర్భస్రావం
Türkmençe: Abort
Tagalog: Pagpapalaglag
Türkçe: Kürtaj
татарча/tatarça: Аборт
українська: Аборт
oʻzbekcha/ўзбекча: Abort
Tiếng Việt: Phá thai
Winaray: Punit
ייִדיש: אבארטאציע
Yorùbá: Ìṣẹ́yún
中文: 堕胎
Bân-lâm-gú: Thu̍t-the
粵語: 落仔