Usimamizi

Usimamizi katika biashara na katika shughuli ya kuwapanga binadamu ni kitendo cha kuwaweka watu pamoja ili kutimiza malengo na madhumuni yatakikanayo. Usimamizi unajumuisha mipango, kuandaa, kuajiri wafanyakazi, kuongoza , na kudhibiti shirika (kundi la mtu mmoja au zaidi au wahusika) au juhudi kwa madhumuni ya kufanikisha lengo. Kugawanya rasilimali kunajumuisha kupelekwa na kutumika kwa rasilimali ya watu, rasilimali ya fedha, rasilimali ya kiteknolojia, na maliasili.

Usimamizi unaweza pia kumrejelea mtu au watu wanaotenda tendo au matendo ya usimamizi.

Historia

Kitenzi simamia (manage) kinatoka katika neno la Kiitaliano maneggiare (kudhibiti- hasa farasi), lugha ambayo kwa upande wake hupata neno hili kutoka Kilatini manus (mkono). Neno la Kifaransa mesnagement (baadaye ménagement) lilichangia maendeleo katika maana ya neno la Kiingereza management katika karne ya 17 na 18. [1]

Baadhi ya ufafanuzi wa usimamizi ni:

  • Mpango na uratibu wa shughuli ya kibiashara kulingana na sera fulani na katika kufanikisha malengo yaliyofafanuliwa vyema. Usimamizi unahusishwa katika vito vya uzalishaji kama vile mashine, vifaa na pesa. Kulingana na gwiji wa usimamizi Peter Drucker (1909-2005), kazi ya msingi ya usimamizi ni mardufu: masoko na uvumbuzi.
  • Wakurugenzi na mameneja ambao wana uwezo na wajibu wa kufanya maamuzi ya kusimamia biashara. Kama nidhamu, usimamizi unajumuisha shughuli zinazohusiana za kubuni sera ya shirika na kuandaa, kupanga, kudhibiti, na kuelekeza rasilimali za kampuni ili kufikia malengo ya sera. Upana wa usimamizi unaweza kuwa kati ya mtu mmoja katika kampuni ndogo hadi mamia au maelfu ya wakurugenzi katika makampuni ya kimataifa. Katika makampuni makubwa, bodi ya wakurugenzi hubuni sera ambayo inatekelezwa na afisa mtendaji mkuu.

Nadharia wigo

Mary Parker Follett (1868-1933), ambaye aliandika juu ya mada hii mapema katika karne ya ishirini, aliufafanua usimamizi kama "sanaa ya kufanya vitu vifanywe kupitia kwa watu". Pia aliuelezea usimamizi kama falsafa. [2] Mtu anaweza kufikiria pia usimamizi kiutendaji, kama hatua ya kupima kiasi mara kwa mara na kurekebisha baadhi ya mipango ya awali; au kama hatua zilizochukuliwa kufikia lengo la mtu. Hii inatumika hata katika hali ambapo kupanga hakufanyiki. Kufuatia mtazamo huu, Mfaransa Henri Fayol [3] anauchukulia usimamizi kuwa na vipengele saba:

  1. Kupanga
  2. kuandaa
  3. Kuongoza
  4. kuratibu
  5. kudhibiti
  6. Kuweka wafanyakazi
  7. kuhamasisha

Baadhi ya watu, hata hivyo, hupata ufafanuzi huu, ingawa ni muhimu, kuwa finyu mno. Msemo "usimamizi ni kile mameneja hufanya" hutokea sana, na kupendekeza ugumu wa kuufafanua usimamizi, asili ya kubadilika badilika ya fasili, na uhusiano wa matendo ya usimamizi na kuwepo kwa viwango au madarasa ya usimamizi.

Tabia moja ya fikra kuhusu usimamizi, inauchukulia kama sawa na "utawala wa biashara " na hivyo haihusishi usimamizi katika maeneo nje ya biashara, kama kwa mfano katika kutoa misaada na katika sekta ya umma. Bayana zaidi, hata hivyo, kila shirika lazima lisimamie kazi yake, watu, taratibu, teknolojia, nk ili kuendeleza kabisa ufanisi wake. Hata hivyo, watu wengi hurejea idara za vyuo vikuu ambavyo hufundisha usimamizi kama "shule za kibiashara." Baadhi ya taasisi (kama Shule ya Biashara ya Harvard) hutumia jina hilo wakati nyingine (kama vile Shule ya Usimizi ya Yale) hutumia neno jumuishi zaidi "usimamizi."

Wazungumzaji wa lugha ya Kiingereza pia huweza kutumia neno "usimamizi" au "kusimamia" kama neno shirkishi linaloeleza mameneja wa shirika, kwa mfano wa Kampuni. Kihistoria matumizi haya ya neno hili, mara nyingi lilitofautishwa na neno "leba" likimaanisha wale wanaosimamiwa.

Asili ya kazi ya usimamizi


Katika kazi za faida, kazi ya msingi ya usimamizi ni kuridhisha makundi mbalimbali ya washikadau. Hii kwa kawaida inahusisha kutengeza faida (kwa wanahisa), kujenga vitu vya thamani kwa gharama ya chini (kwa wateja), na kutoa fursa ya ajira yenye faida (kwa wafanyakazi). Katika usimamizi usio wa faida, kuongeza umuhimu wa kuhifadhi imani ya wafadhili. Katika mifano mingi ya usimamizi / utawala, wanahisa hupigia kura bodi ya wakurugenzi, na kisha bodi inaajiri usimamizi mkuu. Baadhi ya mashirika yamefanya majaribio na njia nyingine (kama mfanyakazi-kupiga kura) ya kuchagua au kubadilisha watawala; lakini hii hutokea tu mara chache sana.

Katika sekta ya umma ya nchi zilizopangwa kama demokrasia ya uwakilishi, wapigaji kura huwapigia kura wanasiasa kwenda afisi ya umma. Wanasiasa hao huwaajiri mameneja na wasimizi wengi, na katika baadhi ya nchi kama Marekani watuele wa kisiasa hupoteza ajira kwa sababu ya uchaguzi wa rais mpya / gavana / meya.

Other Languages
العربية: إدارة
অসমীয়া: ব্যৱস্থাপনা
asturianu: Alministración
azərbaycanca: Menecment
Boarisch: Management
žemaitėška: Vadība
беларуская: Менеджмент
беларуская (тарашкевіца)‎: Мэнэджмэнт
български: Мениджмънт
brezhoneg: Management
bosanski: Menadžment
català: Gestió
čeština: Management
Cymraeg: Rheolaeth
dansk: Ledelse
Deutsch: Management
Ελληνικά: Διαχείριση
English: Management
eesti: Juhtimine
euskara: Kudeaketa
فارسی: مدیریت
français: Management
עברית: ניהול
हिन्दी: प्रबन्धन
hrvatski: Menadžment
magyar: Menedzsment
Bahasa Indonesia: Manajemen
italiano: Management
日本語: 経営管理論
ქართული: მენეჯმენტი
қазақша: Менеджмент
한국어: 경영
Кыргызча: Менеджмент
Limburgs: Bedriefsveuring
lietuvių: Vadyba
latviešu: Vadībzinība
македонски: Менаџмент
монгол: Менежмент
Bahasa Melayu: Pengurusan
Mirandés: Admenistraçon
မြန်မာဘာသာ: စီမံခန့်ခွဲခြင်း
नेपाली: व्यवस्थापन
Nederlands: Management
norsk: Ledelse
Norfuk / Pitkern: Manajement
polski: Zarządzanie
پښتو: سمبالښت
português: Administração
română: Management
русский: Менеджмент
sicilianu: Amministraturi
Scots: Management
srpskohrvatski / српскохрватски: Menadžment
Simple English: Management
slovenčina: Plánovanie
slovenščina: Menedžment
shqip: Menaxhimi
српски / srpski: Руковођење
svenska: Management
தமிழ்: மேலாண்மை
тоҷикӣ: Мудирият
Tagalog: Pamamahala
Türkçe: İşletme
українська: Менеджмент
اردو: نظامت
oʻzbekcha/ўзбекча: Menejment
Tiếng Việt: Quản lý
ייִדיש: פירערשאפט
中文: 管理学
Bân-lâm-gú: Koán-lí-ha̍k