Space Jam

Space Jam
Space jam.jpg
Imeongozwa naJoe Pytka
Imetayarishwa naIvan Reitman
Joe Medjuck
Daniel Goldberg
Imetungwa naLeo Benvenuti
Steve Rudnick
Timothy Harris
Herschel Weingrod
NyotaMichael Jordan
Bugs Bunny
Wayne Knight
Daffy Duck
Lola Bunny
Theresa Randle
Bill Murray
Muziki naJames Newton Howard
Imesambazwa naWarner Bros.
Imetolewa tar.15 Novemba 1996 (Marekani)
Ina muda wa dk.Dakika 88
LughaKiingereza
Bajeti ya filamuDola za US. 80,000,000 US (makadirio)
Mapato yote ya filamuDola za US. 230,418,342

Space Jam ni filamu ya 1996 ya Kimarekani, ambayo imechanganya katuni-na-waigizaji wa kweli, yaani, watu. Ndani ya filamu hii anakuja Michael Jordan, Bugs Bunny (sauti yake imeigizwa na Billy West) na wahusika wengine wote wa Looney Tunes. Filamu ilitayarishwa na Ivan Reitman, na kuongozwa na Joe Pytka (upande wa live-action), Tony Cervone, na Bruce W. Smith (upande katuni). Filamu ilitolewa kwenye maukumbi na Warner Bros. Family Entertainment mnamo 15 Novemba 1996. Filamu inachezwa kivingine kwamba kwanini Michael amerudi tena kwenye mpira wa kikapu, mara hii ameshawishiwa na Bugs Bunny na wenzake.

Hadithi

Akiwa kama nyota wa NBA Michael Jordan amestaafu kucheza mpira wa kikapu ili mradi kujiendeleza zaidi katika micheza baseball, Mister Swackhammer, mmiliki wa hifadhi ya nje ya dunia ya "Moron Mountain", anaomba vivutio vipya kwa ajili ya hifadhi yake inayoanguka. Anatuma watumishi wake, "Nerdlucks", kwenda kuwateka Looney Tunes, ambao wanaishi chini kabisa ya uso wa Dunia. Wakina Looney Tunes wakalipiza kisa kwa kushindana na Nerdlucks kwa mchezo wa mpira wa kikapu (wakionekana kama siyo warefu). Kwa kujianda na mchezo huo, wakina Nerdlucks wakarudi Duniani kuja kuiba vipaji vya kina Charles Barkley, Patrick Ewing, Muggsy Bogues, Larry Johnson na Shawn Bradley. Wakina Nerdlucks wakatumia vipaji walivyoiba kuwa "Mijitu ya Kutisha", viumbe virefu kabisa ambavyo wakina Looney Tunes hawana uwezo wa kushinda wao wenyewe. Kuwashinda wale, wakina Looney Tunes wakamwita Michael Jordan na msaidizi wake Stan Podolak. Baada ya punde, mchezo ukaanza kati ya wakina Looney Tunes na ile Mijitu, lakini wakina Looney Tunes wakaumizwa vibaya-vibaya na mtindo wa uchezaji wa fujo wa ile Mijitu, hivyo haiwezekani mpaka Jordan pekee, Bugs, Lola na Daffy wamebaki wakisimama na kuacha akicheza mtu mmoja tu. Bill Murray, huwa marafiki na mtayarishaji wa filamu, ana uwezo wa kuingia katika ulimwengu wa Looney Tunes na kujiunga na kikosi chao, akatwaa kizuizi. Kileleni mwa mchezo, wakina Tunes wakawa wapo chini kwa moja na juu ya Michael Jordan kushinda pointi ya mwisho kwa ajili ya timu yake. Kwa kutumia mkono wake usio-maarufu na -wenye kurefuka, Michael Jordan ameweza kufanikisha kuweka mpira kwenye kikapu na kushinda mchezo huo. Baada ya hapo, wakina Looney Tunes wakamrudisha Michael Jordan katika sayari yake ya Dunia, ambapo alirejesha kipaji kilichoibiwa kwa wamiliki halisi na kurejea kwelikweli kwenye NBA.

Other Languages
català: Space Jam
čeština: Space Jam
dansk: Space Jam
Deutsch: Space Jam
English: Space Jam
Esperanto: Space Jam
español: Space Jam
euskara: Space Jam
suomi: Space Jam
français: Space Jam
galego: Space Jam
עברית: ספייס ג'אם
Bahasa Indonesia: Space Jam
italiano: Space Jam
한국어: 스페이스 잼
Bahasa Melayu: Filem Space Jam
Nederlands: Space Jam
norsk nynorsk: Space Jam
norsk: Space Jam
português: Space Jam
română: Space Jam
srpskohrvatski / српскохрватски: Space Jam
Simple English: Space Jam
slovenčina: Space Jam
српски / srpski: Свемирски баскет
svenska: Space Jam
Türkçe: Space Jam
українська: Космічний джем
Bân-lâm-gú: Space Jam