Pierce Brosnan

Pierce Brosnan
Pierce Brosnan Deauville 2014.jpg
Bond kwenye Cannes Film Festival, 2002
AmezaliwaPierce Brendan Brosnan
16 Mei 1953 (1953-05-16) (umri 65)
Navan, County Meath, Ireland
Kazi yakeMwigizaji, mtayarishaji
Miaka ya kazi1979–hadi leo
NdoaCassandra Harris
(1977–1991) (kifo chake)
Keely Shaye Smith
(2001–hadi leo)
Tovuti rasmi

Pierce Brendan Brosnan (amezaliwa tar. 16 Mei 1953, Drogheda, Ireland) ni mwigizaji filamu na mtaarishaji wa Kiireland-Marekani. Labda anafahamika zaidi kwa kuigiza kama 'James Bond' katika filamu nne alizocheza kuanzia mwaka 1995 hadi 2002, ambazo ni GoldenEye, Tomorrow Never Dies, The World Is Not Enough na Die Another Day. Tangu atumie jina James bond Brosnan, pia amecheza filamu zingine tofauti ikiwemo ile ya "Evelyn" na "Seraphim Falls".

Pia Brosnan ana kampuni yake inayojishughulisha na maswala ya utengenezaji wa filamu, moja kati ya filamu walizotengeneza ni 'Butterfly on a Wheel, Mamma Mia! na The Topkapi Affair, toka mwaka 1999 alivyo anza ile filamu ya The Thomas Crown Affair.

Maisha ya awali

Brosnan ni Mtoto wa pekee wa Thomas na May, alizaliwa Drogheda, County Louth, Ireland, Brosnan alipelekwa karibu kidogo na mji wa Navan, County Meath ambako huko ndiko alipo kuwa anasoma, alisoma katika shule flani ya kawaida iliyokuwa inaendeshwa na "De La Salle Brothers. Brosnan na Mama yake walihamia mjini London, Uingereza kwa ajili ya kazi baada ya baba yake kuitelekeza familia yake, mwaka 1964, bond alivyofika umri wa miaka kumi na moja baba yake aliirudia familia yake.

Kwa bahati mbaya mama yake akadai taraka, hivyo walikatarikiana na mama yake kuolewa na mzee wa kiingeza alyepigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia mzee William Charmichael, ambaye alimlea Bond kama mwanae wa kumzaa yeye hali ya kuwa ni mtoto wa kufikia.

Charmichael alikuwa wa kwanza kumchukua brosnan na kumpeleka kutazama filamu za James Bond, filamu hiyo ilikuwa ile ya "Gold Finger". Brosnan alisoma katika shule ya 'The Elliot School' ya mjini London, baadae 'secondary modern school', Putney, ilyopo magharibi mwa mji wa London. Brosnan alikuwa na mahusiano ya karibu sana na mwalimu wake wa Jiografia wakati yupo shule anasoma. Alivyomaliza shule jina lake la utani likuwa 'Irish'.

Baada ya masomo Brosnan alitamani sana kuwa msaniii na ndipo alipo anza maelekezo hayo kibiashara katika chuo cha "Central Saint Martins College of Art and Design. Alivyofika umri wa miaka 16 wakala wa sarakasi alimuona Brosnan akachezea moto huku akifanya kama ana ula wakala huyo aka mkodi Brosnan. Baadae alipata mafunzo ya sanaa kwa muda wa miaka mitatu katika chuo cha "The Drama Centre" cha mjini London Uingereza.

Other Languages
Afrikaans: Pierce Brosnan
aragonés: Pierce Brosnan
العربية: بيرس بروسنان
asturianu: Pierce Brosnan
azərbaycanca: Pirs Brosnan
беларуская: Пірс Броснан
български: Пиърс Броснан
čeština: Pierce Brosnan
Ελληνικά: Πιρς Μπρόσναν
Esperanto: Pierce Brosnan
español: Pierce Brosnan
français: Pierce Brosnan
hrvatski: Pierce Brosnan
Հայերեն: Փիրս Բրոսնան
Bahasa Indonesia: Pierce Brosnan
italiano: Pierce Brosnan
Basa Jawa: Pierce Brosnan
қазақша: Пирс Броснан
Lëtzebuergesch: Pierce Brosnan
lietuvių: Pierce Brosnan
latviešu: Pīrss Brosnans
македонски: Пирс Броснан
Bahasa Melayu: Pierce Brosnan
Plattdüütsch: Pierce Brosnan
Nederlands: Pierce Brosnan
português: Pierce Brosnan
română: Pierce Brosnan
русский: Броснан, Пирс
sicilianu: Pierce Brosnan
srpskohrvatski / српскохрватски: Pierce Brosnan
Simple English: Pierce Brosnan
slovenčina: Pierce Brosnan
српски / srpski: Пирс Броснан
Basa Sunda: Pierce Brosnan
Türkçe: Pierce Brosnan
українська: Пірс Броснан
oʻzbekcha/ўзбекча: Pierce Brosnan
Tiếng Việt: Pierce Brosnan
მარგალური: პირს ბროსნანი
Bân-lâm-gú: Pierce Brosnan