Ndizi
English: Banana

Wakulima Watanzania wakibeba shazi la ndizi
Ndizi kwenye mgomba

Ndizi ni tunda muhimu Afrika ya Mashariki na katika nchi za joto kwa jumla hasa visiwa vya caribian. Mmea wake huitwa mgomba. Kibiolojia ndizi moja ni fuu inakua pamoja na fuu nyingine kwenye mshikano au shazi.

Ndizi zapatikana kwa aina nyingi na wataalamu huhesabu takriban 100. Kwa matumizi ya kibinadamu aina zifuatazo zatofautishwa kufuatana na matumizi:

  • Ndizi za kuiva zaliwa kama matunda
  • Ndizi za kupikia zapikwa kama viazi au muhogo
  • Ndizi za uzi yaani magomba hutumiwa kama uzi za kutengezea vitambaa
  • Ndizi za pori siziso na matunda wala matumizi mengine ya chakula

Makabila mengi katika Afrika Mashariki yanaitegemea kama chakula kikuu. Katika kilimo ndizi inatumiwa pia kama lishe ya mifugo na mti wa kivuli katika kilimo cha kahawa.Ndizi

Utangulizi

Ndizi tunda la moja ya mimea ya jenasi ya Musa, ambayo huitwa migomba. Asili yke ni maeneo ya Kusini mwa Asia, na inawezekana kwa mara ya kwanza ilikuzwa huko Papua New Guinea. Leo, ndizi hulimwa maeneo mengi ya tropiki.

matunda ya aina nne ya ndizi

Ndizi zipo katika familia ya Musaceae. Hulimwa hasa kwaajili ya matunda yake, na mara kadhaa kwaajili ya uzalishaji wa nyuzi na kama mimea ya mapambo. Sababu tu mimea ya ndizi, migomba, huwa mirefu na migumu kiasi, huonwa kama ni miti ya kweli, wakati ukweli ni kwamba; kutokana na muundo wa sehemu zake za ndani ya shina migomba si miti ya kweli. Mimea mingi ya aina hii, kitaalamu pseudostem, huweza hata kufikia urefu wa mita 2 – 8, na majani yake hata mpaka urefu wa mita 3.5. na ikikomaa, migomba hutoa mikungu ya ndizi zenye rangi ya kijani ambazo zikiiva hubadilika na kuwa na rangi ya manjano au wakati mwingine hata rangi nyekundu. Kisha kutoa matunda, mgomba hufa na nafasi yake huchukuliwa na mgomba mwingine.

Ndizi hukua kwenye mrindikano mdogo, ujulikanao kama kichana, na kila kichana huwa na ndizi kama 20 hivi huku mkungu mmoja ukuweza kuchukua vichana 3 – 20 kwa wastani. Mkungu unaweza kufkia uzito wa kilo 30 – 50. Ndizi moja kwa wastani huwa na uzito wa gramu 125, ambayo kwa makadirio huwa na maji 75% na mada kavu 25%. Kila ndizi huwa na ganda yenye sehemu laini iliwayo ndani yake. Tena sehemu hiyo ya ndani na maganda huweza kuliwa katika hali ya ubichi au kasha kuiva. Kwa taratibu nyingi za Magharibi, sehemu ya ndani ikiwa mbichi ndiyo hupendelewa kupikwa na kuliwa, huku huko Asia ndizi na maganda yake hupikwa na kuliwa. Tunda la ndizi huwa na nyuzi nyuzi ndani yake, ambazo huwa hasa katikati ya ganda na sehemu laini ya ndani. Sehemu ya laini ya ndani kwa kawaida hugawanyika kwa urahisi kuanzia juu mpaka chini, kwenye sehemu tatu. Ndizi ni chanzo kizuri cha vitamini B6, vitamini C na potasiamu.

[1] ndizi aina ya Cavendish ndio hulimwa kwa wingi.

Ndizi hulimwa katika zaidi ya nchi 107 duniani. katika nchi nyingi, ndizi humaanisha zile laini na tamu ambazo huliwa kama matunda baada yamlo. Lakini pia ndizi zaweza kukatwa na kukaushwa na kuliwa kama vile chipsi. Ndizi zilizokaushwa pia zaweza kusagwa na kupata unga wa ndizi.Ingawa baadhi ya aina ya migomba ya mwituni huwa na ndizi zenye mbegu kubwa na ngumu, ndizi zinazoliwa kwa kawaida huwa hazina mbegu. Kwa kawaida ndizi zote aidha hutumiwa zikiwa zimeiva, za njano na laini au zikiwa mbichi yaani, za kijani na ngumu kiasi. Kwa wastani ndizi zinazouzwa biashara kimataifa ni asilimia 10 – 15 tu, huku Marekani na Uingereza wakiwa wanunuzi wakuu. Maubmile.1.png mmea wa ndizi.

Kitaalamu ndizi huwekwa kwenye jenasi ya Musa katika familia ya Musaceae, kwenye oda ya Zingibrales.

Mmea wake sio mti kamili, huwa na urefu wa mita 6 – 7.6. majani yake hukua kuzunguka mmea na hufukia urefu wa mita 2.7 kwa urefu na sentimita 60 kwa upana. Mgomba ndiyo mmea mkubwa zaidi kuliko mimea mingine ya jamii yake. Majani yake huwa makubwa sana na huchanwa kwa urahisi sana na upepo.

Ua moja la kiume huzalishwa na kila mgomba, japo aina nyingine huweza hata kuzalisha matano ya aina hiyo mfano huko Ufilipino. Maua ya kike huzalishwa juu kabisa mwa shina na baadae hukua na kuwa tunda bila hata ya kurutubishwa. Na katika aina nyingi mbegu zimekuwa dhaifu na haziwezi tena kuzalisha mmea mwingine.

Other Languages
Acèh: Pisang
Afrikaans: Piesang
Alemannisch: Banane
አማርኛ: ሙዝ
aragonés: Banana
العربية: موز
مصرى: موز
অসমীয়া: কল
asturianu: Plátanu
Atikamekw: Pananis
Aymar aru: Puquta
azərbaycanca: Banan
تۆرکجه: موز
башҡортса: Банан
Bikol Central: Batag
беларуская: Банан (плод)
беларуская (тарашкевіца)‎: Банан (плод)
български: Банан (плод)
भोजपुरी: केला
Bislama: Banana
Bahasa Banjar: Pisang
বাংলা: কলা
བོད་ཡིག: ངང་ལག
brezhoneg: Bananez
bosanski: Banana
буряад: Гадил
català: Banana
Mìng-dĕ̤ng-ngṳ̄: Bă-ciĕu
нохчийн: Банан
ᏣᎳᎩ: ᏆᏁᎾ
Tsetsêhestâhese: Vóhka'émene
کوردی: مۆز
corsu: Banana
čeština: Banán
kaszëbsczi: Banan
Cymraeg: Banana
dansk: Banan
ދިވެހިބަސް: ދޮންކެޔޮ
eʋegbe: Akɔɖu
Ελληνικά: Μπανάνα
English: Banana
Esperanto: Banano
español: Banana
eesti: Banaan
euskara: Banana
فارسی: موز
suomi: Banaani
français: Banane
Gaeilge: Banana
贛語: 香蕉
Gàidhlig: Banana
galego: Banana
ગુજરાતી: કેળાં
Gaelg: Bananey
客家語/Hak-kâ-ngî: Khiûng-chiâu
עברית: בננה (פרי)
हिन्दी: केला
Fiji Hindi: Jaina
hornjoserbsce: Banana
Kreyòl ayisyen: Bannann
magyar: Banán
հայերեն: Բանան
interlingua: Banana (fructo)
Bahasa Indonesia: Pisang
Ilokano: Saba
Ido: Banano
íslenska: Banani
italiano: Banana
日本語: バナナ
la .lojban.: badna
Basa Jawa: Gedhang
қазақша: Банан
ភាសាខ្មែរ: ចេក
한국어: 바나나
कॉशुर / کٲشُر: کیل
kurdî: Mûz
Кыргызча: Банан
lumbaart: Musa
lingála: Etabé
latviešu: Banāni
Basa Banyumasan: Gedhang
Malagasy: Akondro
Baso Minangkabau: Pisang
македонски: Банана
മലയാളം: വാഴ
монгол: Гадил
मराठी: केळ
Bahasa Melayu: Pisang
မြန်မာဘာသာ: ငှက်ပျော
नेपाली: केरा
नेपाल भाषा: म्वाय्
Nederlands: Banaan (vrucht)
norsk nynorsk: Banan
norsk: Bananer
Sesotho sa Leboa: Panana
occitan: Banana
ଓଡ଼ିଆ: କଦଳୀ
ਪੰਜਾਬੀ: ਕੇਲਾ
Kapampangan: Sagin
polski: Banan (owoc)
پنجابی: کیلا
پښتو: كيله
português: Banana
русский: Банан
русиньскый: Банан
Kinyarwanda: Umuneke
संस्कृतम्: कदलीफलम्
ᱥᱟᱱᱛᱟᱲᱤ: ᱠᱟᱭᱨᱟ
sardu: Banana
sicilianu: Banana
Scots: Bananae
سنڌي: ڪيلو
srpskohrvatski / српскохрватски: Banana
සිංහල: කෙසෙල්
Simple English: Banana
slovenčina: Banán
slovenščina: Banana
Gagana Samoa: Fa'i
Soomaaliga: Moos
shqip: Bananja
српски / srpski: Банана
Basa Sunda: Cau
svenska: Banan
తెలుగు: అరటి
тоҷикӣ: Банан (мева)
ไทย: กล้วย
Tagalog: Saging
Setswana: Banana
Tok Pisin: Banana
Türkçe: Muz
chiTumbuka: Ntochi
reo tahiti: Meià
українська: Банан (плід)
اردو: کیلا
oʻzbekcha/ўзбекча: Banan
Tiếng Việt: Chuối
West-Vlams: Bananne
Volapük: Benen
Winaray: Saging
Wolof: Banaana
吴语: 香蕉
ייִדיש: באנאן
Vahcuengh: Gyoijhom
中文: 香蕉
Bân-lâm-gú: Kin-chio
粵語: 香蕉