Mein Kampf

Toleo la Kifaransa la "Mein Kampf".

Mein Kampf (tamka main kampf; maana ya Kijerumani: Mapambano au mapigano yangu) ni kitabu kilichoandikwa na Adolf Hitler kabla ya kushika utawala wa Ujerumani. Alieleza humo mawazo yake juu ya siasa, historia na dunia kwa jumla.

Hitler aliandika kitabu cha kwanza cha Mein Kampf gerezani alipofungwa baada ya jaribio la kupindua serikali mwaka 1923. Alipoondoka aliongeza kitabu cha pili. Tangu mwaka 1930 sehemu zote mbili zilichapishwa pamoja kama kitabu kimoja.

Katika kitabu chake Hitler alieleza kwa upana mawazo yake mbalimbali.

Yaliyomo yalikuwa

  1. alidai maungano ya Austria na Ujerumani
  2. alieleza kwa upana uadui wake dhidi ya Wayahudi akidai waliendesha ubepari lakini pia kinyume chake yaani ukomunisti kwa shabaha ya kutawala dunia. Hapo ulikuwa msingi wa siasa yake iliyochocheza uadui dhidi ya kundi dogo alilodai kuwa sababu ya maovu yote.
  3. alitangaza ujamaa au usoshalisti wa kitaifa badala ya ujamaa wa kimataifa akilenga tabaka kubwa la wafanyakazi wa viwandani;
  4. alieleza utawala wa ukomunisti katika Urusi ulipaswa kuondolewa kwa vita
  5. alidai ardhi mashariki mwa Ulaya ilihitajika kwa ajili ya Wajerumani ambao aliwaona walikosa nafasi waliostahili,
  6. alikashifu demokrasia kama muundo wa serikali na dola akidai ya kwamba utamaduni asilia wa Wajerumani ni kuwa na kiongozi mwenye mamlaka yote

Kitabu kilitangazwa kama "biblia" ya harakati ya Manazi. Baada ya Hitler kuwa kiongozi wa serikali na dikteta kilichapishwa na kugawiwa na vyombo vya serikali; bwana na bibi arusi wote walipewa nakala. Kwa jumla kilitolewa zaidi ya mara milioni kumi.

Baada ya mwisho wa utawala wake mwaka 1945 kitabu kilipigwa marufuku katika Ujerumani hadi leo. Mtu anaruhusiwa kuwa nacho lakini hakuna ruhusa kukichapisha upya.

Other Languages
Afrikaans: Mein Kampf
العربية: كفاحي (كتاب)
مصرى: كفاحى
azərbaycanca: Mein Kampf
Bikol Central: Mein Kampf
беларуская: Мая барацьба
български: Моята борба
bosanski: Mein Kampf
català: Mein Kampf
Cebuano: Mein Kampf
čeština: Mein Kampf
Cymraeg: Mein Kampf
dansk: Mein Kampf
Deutsch: Mein Kampf
Ελληνικά: Ο Αγών μου
English: Mein Kampf
Esperanto: Mein Kampf
español: Mi lucha
eesti: Mein Kampf
euskara: Mein Kampf
فارسی: نبرد من
suomi: Taisteluni
français: Mein Kampf
Gaeilge: Mein Kampf
galego: Mein Kampf
हिन्दी: मीन कैम्फ
hrvatski: Mein Kampf
magyar: Mein Kampf
հայերեն: Իմ պայքարը
Bahasa Indonesia: Mein Kampf
íslenska: Mein Kampf
italiano: Mein Kampf
日本語: 我が闘争
Basa Jawa: Mein Kampf
ქართული: ჩემი ბრძოლა
한국어: 나의 투쟁
Latina: Mein Kampf
Lingua Franca Nova: Mein Kampf
lietuvių: Mano kova
latviešu: Mana cīņa
македонски: Мојата борба
Bahasa Melayu: Mein Kampf
Mirandés: Mein Kampf
Nederlands: Mein Kampf
norsk: Mein Kampf
occitan: Mein Kampf
polski: Mein Kampf
português: Mein Kampf
română: Mein Kampf
armãneashti: Mein Kampf
русский: Моя борьба
Scots: Mein Kampf
srpskohrvatski / српскохрватски: Mein Kampf
Simple English: Mein Kampf
slovenčina: Mein Kampf
slovenščina: Moj boj
shqip: Mein Kampf
српски / srpski: Мајн кампф
svenska: Mein Kampf
Tagalog: Mein Kampf
Türkçe: Kavgam
українська: Моя боротьба
Tiếng Việt: Mein Kampf
ייִדיש: מיין קאמף
Zeêuws: Mein Kampf
中文: 我的奋斗
Bân-lâm-gú: Mein Kampf