Maximilian Kolbe

Karatasi ya maombezi yenye mchoro wa Mtakatifu Maximilian Kolbe akimuomba Bikira Maria Imakulata huku amefungwa katika kambi la Wanazi.

Maximilian Maria Kolbe (8 Januari 189414 Agosti 1941) alikuwa padre wa Kanisa Katoliki na mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo Wakonventuali kutoka nchi ya Poland.

Katika historia ya Kanisa anajulikana kwa jinsi allivyomheshimu Bikira Maria kwa jina la Imakulata, yaani Mkingiwa dhambi asili.

Baada ya kuanzisha chama cha Mashujaa wa Imakulata huko Roma (Italia) na Mji wa Imakulata huko Polandi, alikwenda Japani kama mmisionari.

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia alifungwa na wafuasi wa Nazi katika kambi ya wafungwa wa siasa kule Auschwitz. Hatimaye alijitolea kushika nafasi ya mfungwa mwenzake aliyechaguliwa kuachwa bila ya chakula hadi kufa pamoja na wengine 9. Aliwaandaa hao wote kukabili kifo kwa tumaini la Kikristo na bila ya chuki, na alipobaki peke yake aliuawa kwa sindano ya sumu.

Mwaka 1982 alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mtakatifu mfiadini. Sikukuu yake ni tarehe 14 Agosti kila mwaka.

Other Languages
беларуская: Максімілян Кольбэ
čeština: Maxmilián Kolbe
français: Maximilien Kolbe
गोंयची कोंकणी / Gõychi Konknni: Maximilian Kolbe
Bahasa Indonesia: Maximilian Kolbe
Nederlands: Maximiliaan Kolbe
Simple English: Maximilian Kolbe
slovenčina: Maximilián Kolbe
slovenščina: Maksimilijan Kolbe
Tiếng Việt: Maximilian Kolbe