
Ulinganifu wa masi za nyota: nyota kibete nyekundu (M
☉ 0.1), Jua, nyota kibete buluu (M
☉ 8) na R136a (M
☉ 300)
Masi ya Jua (ing. Solar mass) inataja masi ya Jua letu ambayo ni takriban kilogramu 1.99 × 1030 . Hi inalingana na masi za Dunia yetu mara 332,946.
Kiwango hiki hutumiwa kama kizio katika sayansi ya astronomia kwa kutaja masi ya magimba kwenye anga la nje hasa nyota, fungunyota na galaksi.
Nyota nyingi huwa na masi baina ya x0.1 na x10 ya masi ya Jua. Mara chache kuna nyota kubwa sana yenye masi x250 za Jua. Hivyo Jua letu iko kwenye wastani ya masi za nyota kati ya nyota za safu kuu.
Ilhali masi ya Jua inaendelea kupungua polepole kutokana na mnururisho na upepo wa Jua kuna ufafanuzi wa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia wa kuhesabu masi ya Jua kuwa kilogramu 1.9891×1030[1].
Alama yake ni M☉ ambako "M" inamaanisha "masi" na ☉ ni ishara ya Jua.