Manowari
English: Warship

Manowari ya Assyria takriban mwaka 700 BK
Uchoraji wa Willem van der Velde unaonyesha manowari ya kiholanzi ya karne ya 17
Manowari ya Kiingereza HMS Dreadnought yenye injini ya mvuke na mizinga mikubwa ilijengwa mwaka 1906
USS Vandegrift ikirusha kombora ni manowari ya kisasa

Manowari ni meli yenye silaha iliyojengwa kwa kusudi la kuitumia katika vita.

Asili ya neno "manowari" ni kiing. "man-of-war" au kifupi chake "man-o'-war" (mtu wa vita) ambacho ni Kiingereza cha karne za 16 hadi 19 BK kinachotaja hasa jahazi kubwa ya kivita lakini pia jahazi au meli yoyote ya kivita.

Muundo wa manowari

Muundo wake huwa ni tofauti na meli zinazokusudiwa kubeba mizigo au watu.

Tabia muhimu za manowari ni kasi na kinga pamoja na uwezo wa kubeba silaha. Hasa tabia za kasi na kinga zimeshindana mara nyingi katika historia ya ujenzi ya meli hizi.

Manowari inaweza kukingwa dhidi ya silaha kwa kuweka mabamba mazito ya metali nje ya bodi yake au kujenga bodi yake moja kwa moja kwa kutumia metali nzito. Ila tu kinga inaongeza uzito na kupunguza mkasi; kwa hiyo manowari yenye kinga mzuri inaweza kuwa lengo la silaha za adui kwa sababu mwendo wake ni polepole mno.

Manowari yenye kasi kubwa inahitaji kupunguza uzito wake hivyo haiwezi kujikinga vile. Ikipigwa na silaha za adui inazama haraka lakini faida yake ni mwendo unaoepukana na kupigwa.

Mara nyingi katika historia kutokea kwa aina mpya ya kinga kulibatilisha silaha za mashambulio yaliyokuwepo. Lakini baadaye silaha mpya ziliweza kutoboa kinga mpya na kulibatilisha. Hadi sasa imekuwa mashindano ya kurudiarudia.

Other Languages
aragonés: Vaixiello
العربية: سفينة حربية
asturianu: Buque de guerra
беларуская: Карабель
bosanski: Ratni brod
čeština: Válečná loď
Чӑвашла: Карап
dansk: Krigsskib
Deutsch: Kriegsschiff
Ελληνικά: Πολεμικό πλοίο
English: Warship
Esperanto: Militoŝipo
español: Buque de guerra
eesti: Sõjalaev
euskara: Gerraontzi
فارسی: کشتی جنگی
suomi: Sota-alus
français: Navire de guerre
Gaeilge: Long chogaidh
हिन्दी: युद्धपोत
hrvatski: Ratni brod
հայերեն: Ռազմանավ
Bahasa Indonesia: Kapal perang
íslenska: Herskip
日本語: 軍艦
қазақша: Кеме
한국어: 군함
Lëtzebuergesch: Krichsschëff
Lingua Franca Nova: Barcon de gera
lietuvių: Karo laivas
Bahasa Melayu: Kapal perang
norsk nynorsk: Krigsskip
norsk: Krigsskip
पालि: Nāvā
polski: Okręt
português: Navio de guerra
română: Navă militară
русский: Корабль
Scots: Warship
srpskohrvatski / српскохрватски: Ratni brod
Simple English: Warship
slovenčina: Vojnová loď
slovenščina: Vojne ladje
shqip: Luftanija
српски / srpski: Ратни брод
svenska: Stridsfartyg
తెలుగు: యుద్ధనౌక
Türkçe: Savaş gemisi
українська: Корабель
Tiếng Việt: Tàu chiến
中文: 军舰
Bân-lâm-gú: Kun-lām
粵語: 戰船