Kisukuku

Kiunzi cha mifupa cha Ichthyosauria (sauri ya bahari) kilichopatikana Ujerumani kusini aliyeishi takriban miaka milioni 200 - 100 iliyopita
Trilobiti walikuwa viumbe vya miaka milioni 444 iliyopita.
Mti uliokuwa jiwe
Archeopteryx ni ndege wa kwanza anayejulikana kutokana na visukuku akifanana bado na reptilia lakini anaonyesha manyoa tayari

Kisukuku (kwa Kiingereza: fossile) ni mabaki ya kiumbehai (mmea au mnyama) kutoka zamani za miaka 10,000 au zaidi. Visukuku vingi vina umri wa miaka milioni kadhaa.

Mabaki yanapatikana kwa umbo tofautitofauti, hasa kama:

  • visukuku vya kijiwe vinavyoweza kutupa picha ya viumbehai vya nyakati zilizopita, na
  • visukuku vya makaa na mafuta ambavyo ni chanzo muhimu cha nishati.

Visukuku vya kijiwe

Mara nyingi miili ya wanyama na mimea imehifadhiwa kwa umbo la jiwe. Ni kama picha au hata sanamu ya kiumbe kile. Mifano bora imepatikana pale ambapo mmea au mwili wa mnyama ulianguka katika matope laini na kuzama chini haraka. Ndani ya matope laini mwili haukuoza shauri la uhaba wa oksijeni na uhaba wa bakteria. Polepole maji ya matope yaliingia ndani ya mwili na kujaza nafasi zilizojazwa awali na kiowevu cha seli wakati kiumbe kilipokuwa hai. Maji ya matope yalipeleka pia minerali mbalimbali ndani ya mwili. Jinsi mwendo huu ulivyoweza kuendelea bila kuzuiwa, polepole hata seli ziliweza kujazwa kwa vipande vidogo vya matope na minerali nyingine. Kama baada ya miaka mingi matope yalikauka, hata matope ndani ya seli za mwili ulikauka lakini kwa kutunza umbo la seli hizi. Kama ganda la matope liliendelea kufunikwa na tabaka za udongo wa juu, shindikizo la juu lilianza kubadilisha ule udongo kuwa jiwe na mwamba kabisa.

Kama mwili wenyewe umeshaoza hadi kiunzi cha mifupa kilifunikwa kuna pia visukuku vya mifupa tu. Viumbe kama konokono mara nyingi viliacha visukuku vya umbo la nje pekee, kwa sababu miili yao ni laini sana, hivyo ilipotea haraka, na ganda lao halikubali maji yenye minerali kuingia ndani yake.

Sehemu ambako mazingira yalifaa kwa kutokea kwa visukuku huitwa na wataalamu "Lagerstätte" (la-ger-ste-te, neno la Kijerumani) na hapa mifano mingi imewahi kuchimbwa. Kutokana na mwendo wa gandunia (yaani kukunjwa kwa ganda la dunia) sehemu hizi zinaweza kupatikana chini ya ardhi au juu mlimani.

Kwa njia hii ilitokea mifano kamili ya miili ya spishi zisizopatikana tena duniani. Wataalamu hulinganisha visukuku na wanyama au mimea ya leo na hapo wanapata picha juu ya mabadiliko ya spishi. Nadharia ya mageuko ya spishi iliathiriwa sana na matokeo ya utafiti wa visukuku.

Aina ya pekee ya visukuku ni wadudu waliofungwa ndani ya utomvu wa miti uliobadilika baadaye kuwa kaharabu.

Other Languages
Afrikaans: Fossiel
Alemannisch: Fossil
العربية: مستحاثة
asturianu: Fósil
azərbaycanca: Fosil
تۆرکجه: فوسیل
беларуская: Акамянеласці
български: Вкаменелост
বাংলা: জীবাশ্ম
brezhoneg: Karrekaenn
bosanski: Fosili
català: Fòssil
Mìng-dĕ̤ng-ngṳ̄: Huá-siŏh
čeština: Fosilie
Cymraeg: Ffosil
dansk: Fossil
Deutsch: Fossil
Ελληνικά: Απολίθωμα
English: Fossil
Esperanto: Fosilio
español: Fósil
eesti: Kivistis
euskara: Fosil
فارسی: سنگواره
suomi: Fossiili
français: Fossile
Frysk: Fossyl
Gaeilge: Iontaise
galego: Fósil
עברית: מאובן
हिन्दी: जीवाश्म
hrvatski: Fosil
Kreyòl ayisyen: Fosil
magyar: Fosszília
Bahasa Indonesia: Fosil
Ido: Fosilo
íslenska: Steingervingur
italiano: Fossile
日本語: 化石
Basa Jawa: Fosil
қазақша: Қазындылар
한국어: 화석
Latina: Fossile
Lëtzebuergesch: Fossil
Limburgs: Fossiel
lietuvių: Fosilija
latviešu: Fosilijas
Basa Banyumasan: Fosil
македонски: Фосил
മലയാളം: ജീവാശ്മം
मराठी: जीवाश्म
Bahasa Melayu: Fosil
Plattdüütsch: Fossil
नेपाली: जीवावशेष
Nederlands: Fossiel
norsk nynorsk: Fossil
norsk: Fossil
occitan: Fossil
ଓଡ଼ିଆ: ଜୀବାଶ୍ମ
ਪੰਜਾਬੀ: ਪਥਰਾਟ
português: Fóssil
Runa Simi: Rumiyasqa
română: Fosilă
русский: Фоссилии
Scots: Fossil
سنڌي: فاسل
srpskohrvatski / српскохрватски: Fosil
සිංහල: පොසිල
Simple English: Fossil
slovenčina: Fosília
slovenščina: Fosil
shqip: Fosilet
српски / srpski: Фосил
Basa Sunda: Fosil
svenska: Fossil
తెలుగు: శిలాజము
Tagalog: Posil
Türkçe: Fosil
اردو: رکاز
Tiếng Việt: Hóa thạch
West-Vlams: Fossiel
Winaray: Posil
ייִדיש: פאסיל
中文: 化石
Bân-lâm-gú: Hòa-chio̍h
粵語: 化石