Kipimaanga

Kipimaanga Rosetta kikikaribia nyotamkia 67P/Churyumov–Gerasimenko kwenye mwaka 2014.

Kipimaanga (kutoka maneno kupima na anga, kwa Kiingereza space probe) ni chombo cha angani kisichobeba watu na kutumwa katika anga ya nje kwa kusudi la kukusanya data na kutekeleza vipimo vya sayari, miezi, Jua au violwa vya angani kwa jumla.

Tofauti na satelaiti, haizunguki Dunia bali inafuata njia iliyopangwa nje ya uga wa graviti ya Dunia..

Kuna aina mbalimbali za vipimaanga kama vile

  • kipimaanga kinachopita karibu na gimba la angani kwa kusudi la kupiga picha na kukusanya data zake na za mazingira yake
  • kipimaanga kunachoingia katika njiamzingo ya kuzunguka gimba la angani inapoendelea kukusanya data zake kwa muda mrefu kiasi
  • kipimaanga kinachotua kwenye uso wa gimba la angani
  • kipimaanga kinachorudi duniani baada ya kukusanya sampuli za mata ya gimba la angani, angahewa yake au vyembe kutoka anga la nje

Kipimaanga cha kwanza kilikuwa Luna 1 ya Umoja wa Kisovyeti kilichopita karibu na Mwezi kwenye Januari 1959. Kilikusanya data kuhusu Ukanda wa van Allen na kuthibitisha kuwepo kwa upepo wa Jua.

Vipimaanga vya baadaye vilifika kwenye uso wa Mwezi na Mirihi, vilipita karibu na sayari zote nyingine hadi mwisho wa mfumo wa Jua.

Chombo kilichosafiri mbali kabisa ni Voyager 1 iliyorushwa angani kwenye mwaka 1977 na kwenye Januari 2018 imeshapita obiti ya Pluto na kufikia umbali wa kilomita bilioni 21 kutoka kwenye Jua.

Astrowiki.PNG
Mradi wa Astronomia

Makala hii imewahi kukaguliwa na kuboreshwa kwenye warsha ya pamoja ya Jenga Wikipedia ya Kiswahili, Wikimedia Community User Group Tanzania na ASSAT. Imepewa hali ya ulinzi. Tunaomba mapendekezo yote ya usahihisho na nyongeza zipelekwe kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano

Other Languages
Alemannisch: Raumsonde
العربية: مسبار فضائي
asturianu: Sonda espacial
беларуская (тарашкевіца)‎: Аўтаматычная міжплянэтная станцыя
čeština: Kosmická sonda
dansk: Rumsonde
Deutsch: Raumsonde
English: Space probe
Esperanto: Kosmosondilo
español: Sonda espacial
euskara: Espazio zunda
français: Sonde spatiale
Nordfriisk: Rümsonde
עברית: גשושית
Kreyòl ayisyen: Sonn espasyal
magyar: Űrszonda
Bahasa Indonesia: Prob antariksa
íslenska: Könnunarfar
italiano: Sonda spaziale
日本語: 宇宙探査機
한국어: 우주 탐사선
Lëtzebuergesch: Raumsond
lietuvių: Kosminis zondas
Bahasa Melayu: Kuar angkasa lepas
Plattdüütsch: Ruumsond
Nederlands: Ruimtesonde
norsk nynorsk: Romsonde
norsk: Romsonde
ਪੰਜਾਬੀ: ਪੁਲਾੜ ਟਟੋਲ
português: Sonda espacial
srpskohrvatski / српскохрватски: Svemirska sonda
Simple English: Space probe
slovenčina: Kozmická sonda
slovenščina: Vesoljska sonda
српски / srpski: Свемирска сонда
svenska: Rymdsond
Türkçe: Uzay sondası
Tiếng Việt: Thăm dò không gian