Kamba (gegereka)

Kamba
Kamba mwilo (Panulirus longipes)
Kamba mwilo (Panulirus longipes)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya:Animalia (Wanyama)
Faila:Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila:Crustacea (Arthropoda wenye miguu yenye matawi mawili)
Ngeli:Malacostraca (Crustacea wenye sehemu tatu)
Oda:Decapoda (Crustacea wenye miguu mikumi)
Ngazi za chini

Nusuoda 2 na oda za chini 10:

 • Dendrobranchiata
 • Pleocyemata
  • Achelata
  • Anomura
  • Astacidea
  • Axiidea
  • Brachyura (Siyo kamba lakini kaa)
  • Caridea
  • Gebiidea
  • Glypheidea
  • Polychelida
  • Stenopodidea

Kamba ni wanyama wa faila Arthropoda na oda Decapoda (kutoka Kiyanuni Δεκάποδα: δέκα = kumi, πούς, ποδός = mguu), lakini spishi za oda ya chini Brachyura huitwa kaa. Spishi ndogo huwa na majina kama uduvi, duvi, kijino na ushimbu.

Mwili wa kamba una sehemu mbili: kefalotoraksi (kichwa na kidari vilivyoungana) na fumbatio. Kwa hivyo kamba wana miguu kumi, jozi tano za viungo vya kefalotoraksi, vinavyoitwa pereiopodi pia. Lakini kila pingili ya mwili inaweza kuwa na jozi ya viungo, ijapokuwa vingine vimepotea katika spishi nyingi. Vile vya kichwa ni vipapasio vidogo na vikubwa, mandibuli na maxilla za kwanza na za pili. Jozi ya kwanza ya miguu inabeba magando, pengine madogo pengine makubwa. Kidari kinabeba jozi tatu za viungo mbele ya miguu ambavyo vinaitwa maxillipedi. Viungo hivi vinasaidia kwa kula.

Fumbatio inabeba idadi mbalimbali za viungo vinavyoitwa pleopodi na ambovyo vinatumika kwa kuogelea na kuatamia mayai. Kwa spishi nyingine jozi ya kwanza, na pengine jozi ya pili pia, ya madume imetoholeka ili kumwekea jike manii. Viungo vya pingili ya mwisho huitwa uropodi na mwishoni kwa fumbatio kuna telsoni. Uropodi na telsoni pamoja zinaumba kipepeo cha mkia kinachotumika kwa kutimuka kikikunjwa kwa kasi.

 • spishi za afrika mashariki zilizochaguliwa
 • picha

Spishi za Afrika Mashariki zilizochaguliwa

 • Aristaeomorpha foliaceae, Kamba mwekundu mkubwa
 • Aristaeopsis edwardsiana, Kamba mwekundu
 • Linuparus somniosus, Kambamawe mkuki
 • Metanephros andamanicus, Kambamawe wa Andamani
 • Metanephron mozambicus, Kambamawe wa Msumbiji
 • Nephropsis stewarti, Kambamawe wa Stewart
 • Nematopalaemon tenuipes, Kamba-buibui
 • Panulirus homarus, Kamba springi
 • Panulirus longipes, Kamba mwilo
 • Panulirus ornatus, Kamba mwani
 • Panulirus penicillatus, Kamba kijiwe
 • Panulirus versicolor, Kambakurabu
 • Penaeus monodon, Kambamti mkubwa
 • Penaeus semisulcatus, Kambamti kijani
 • Puerulus angulatus, Kambamawe milia
 • Scyllarides squammosus, Kamba-mzuka butu
 • Scyllarides tridacnophaga, Kamba-mzuka mlashaza
 • Scyllarus batei, Kamba-mzuka laini
 • Scyllarus rugosus, Kamba-mzuka kibyongo
 • Thenus orientalis, Kamba-mzuka kichwa-bapa
Other Languages
Afrikaans: Tienpotiges
asturianu: Decapoda
azərbaycanca: Onayaqlılar
беларуская (тарашкевіца)‎: Дзесяціногія ракападобныя
български: Десетоноги
brezhoneg: Decapoda
català: Decàpodes
Mìng-dĕ̤ng-ngṳ̄:
Cebuano: Decapoda
čeština: Desetinožci
Ελληνικά: Δεκάποδα
English: Decapoda
Esperanto: Dekpieduloj
español: Decapoda
euskara: Decapoda
فارسی: ده‌پایان
français: Decapoda
Gaeilge: Decapoda
galego: Decápodos
hrvatski: Deseteronošci
interlingua: Decapoda
Bahasa Indonesia: Dekapoda
italiano: Decapoda
日本語: 十脚目
한국어: 십각목
kurdî: Dehpê
Latina: Decapoda
Lingua Franca Nova: Decapoda
latviešu: Desmitkājvēži
മലയാളം: ഡെക്കാപോഡ
Nederlands: Tienpotigen
norsk nynorsk: Tifotkreps
norsk: Tifotkreps
occitan: Decapoda
português: Decapoda
Scots: Decapoda
srpskohrvatski / српскохрватски: Deseteronošci
Simple English: Decapod
slovenčina: Desaťnožce
slovenščina: Deseteronožci
српски / srpski: Decapoda
Tagalog: Decapoda
lea faka-Tonga: Veʻehongofulu
українська: Десятиногі
اردو: دسپا
Tiếng Việt: Giáp xác mười chân
Winaray: Decapoda
中文: 十足目
Bân-lâm-gú: Cha̍p-kha-ba̍k
粵語: 十腳目