Jacques Maritain

Jacques Maritain (Paris, 18 Novemba 1882 – 28 Aprili 1973) alikuwa mwanafalsafa kutoka Ufaransa.

Maisha yake

Kisha kulelewa katika Uprotestanti, aliasi dini na kuona haiwezekani kujua kama Mungu yupo kweli.

Wakati wa masomo yake ya sayansi katika chuo kikuu cha Sorbonne, Paris, alikutana na Raïssa Oumançoff, Myahudi kutoka Urusi.

Walipoona elimu haijibu maswali makuu juu ya maana ya maisha, mwaka 1901 walikubaliana kujiua kwa wakati mmoja. Lakini waliepushwa na rafiki yao aliyewaelekeza kufuata vipindi vya wanafalsafa bora.

Mwaka 1904 walioana na mwaka 1906 waliongokea Kanisa Katoliki.

Baada ya hapo wote wawili waliandika sana. Jacques alitunga zaidi ya vitabu 60, akisaidia kufufua mafundisho ya Thomas Aquinas na kutunga Tamko la kimataifa la haki za binadamu.

Mwishoni mwa Mtaguso II wa Vatikano, Papa Paulo VI alimkabidhi yeye "Ujumbe kwa Wanafalsafa na Wanasayansi".

Baada ya kufiwa mke wake, alikwenda kuishi utawani hadi kifo chake mwenyewe.

Other Languages
العربية: جاك ماريتان
azərbaycanca: Jak Mariten
беларуская: Жак Марытэн
čeština: Jacques Maritain
français: Jacques Maritain
Հայերեն: Ժակ Մարինետ
Bahasa Indonesia: Jacques Maritain
қазақша: Жак Маритен
한국어: 자크 마리탱
Nederlands: Jacques Maritain
Piemontèis: Jacques Maritain
português: Jacques Maritain
русский: Маритен, Жак
slovenčina: Jacques Maritain
slovenščina: Jacques Maritain
українська: Жак Марітен