Gambia (mto)

Mto Gambia
Mto Gambia kutoka angani - mstari mweusi ni mipaka ya nchi ya Gambia.
ChanzoNyanda za juu za Futa Djalon, Guinea
MdomoAtlantiki kwa mji wa Banjul
NchiGuinea, Senegal & Gambia
Urefu1,120 km
Kimo cha chanzo900 m takriban
Mkondohadi 2000 m³/s kutegemeana na majira na kiasi cha mvua njiani
Eneo la beseni69,931 hadi 87,850 km² (maelezo hutofautiana)

Gambia ni mto unaoanza katika milima ya Futa Djalon huko Guinea. Unafuata njia ya kunyoka hadi Atlantiki. Mdomo wake ni pana sana.

Baada ya kutoka katika Futa Djallon mto unaelekea kaskazini-magharibi kupitia mkoa wa Tambakunda katika Senegal halafu mbuga wa wanyama wa Niokolo Koba. Hapa inapokea tawimiti ya Nieri Ko and Kuluntu na kuingia katika nchi ya Gambia karibu na mji wa Fatoto.

Mto Gambia ukipitia mbuga wa Niokolo-Koba nchini Senegal

Kuanzia hapa mto unaelekea magharibi tu isipokuwa kwa njia ya kunyokanyoka. Takriban km 100 kabla ya kufika mdomo unaanza kupanuka ukiwa na upana wa km 10 mdomoni penyewe.

Mto una visiwa mbalimbali ndani yake, vikubwa zaidi ni kisiwa cha Tembo na kisiwa cha MacCarthy. Kisiwa cha James Island mdomoni kabisa kilikuwa kituo muhimu cha biashara ya watumwa na kimeandikishwa katika orodha ya UNESCO ya Urithi wa Dunia.

Kutokana na upana na wingi wa maji Gambia inafaa kama njia ya maji; meli za baharini zinaingia ndani takriban km 280.

Miji mikubwa zaidi mtoni ni Basse Santa Su, Janjanbureh na Banjul.

Other Languages
Afrikaans: Gambiërivier
العربية: نهر غامبيا
asturianu: Ríu Gambia
تۆرکجه: قامبیا چایی
беларуская: Гамбія (рака)
беларуская (тарашкевіца)‎: Гамбія (рака)
български: Гамбия (река)
brezhoneg: Gambia (stêr)
català: Riu Gàmbia
čeština: Gambie (řeka)
Cymraeg: Afon Gambia
English: Gambia River
Esperanto: Rivero Gambio
español: Río Gambia
français: Gambie (fleuve)
galego: Río Gambia
Avañe'ẽ: Ysyry Gámbia
հայերեն: Գամբիա (գետ)
Bahasa Indonesia: Sungai Gambia
italiano: Gambia (fiume)
日本語: ガンビア川
Basa Jawa: Kali Gambia
한국어: 감비아강
Lëtzebuergesch: Gambia (Floss)
lietuvių: Gambija (upė)
latviešu: Gambija (upe)
македонски: Гамбија (река)
Bahasa Melayu: Sungai Gambia
Nederlands: Gambia (rivier)
norsk nynorsk: Gambiaelva
português: Rio Gâmbia
română: Fluviul Gambia
русский: Гамбия (река)
srpskohrvatski / српскохрватски: Gambija (rijeka)
Simple English: Gambia River
slovenčina: Gambia (rieka)
slovenščina: Gambija (reka)
српски / srpski: Гамбија (река)
svenska: Gambiafloden
Tagalog: Ilog Gambia
Türkçe: Gambiya Nehri
українська: Гамбія (річка)
Tiếng Việt: Sông Gambia
中文: 冈比亚河