Funguvisiwa ya Franz Josef

Ramani ya funguvisiwa ya Franz Josef
Mahali pa Nchi ya Franz Josef kwenye Aktiki

Funguvisiwa ya Franz Josef au Nchi ya Franz Josef (au Funguvisiwa/Nchi ya Frants Iosif) ni funguvisiwa upande wa kaskazini ya Novaya Zemlya katika Bahari Aktiki. Ni sehemu ya Urusi na kuhesabiwa kama sehemu ya mkoa wa Arkhangelsk Oblast. Ni kundi la visiwa 191.

Ni eneo baridi sana. Usafiri wa kwenda wa kuondoka unapatikana kwenye wiki chache cha majirajoto pekee. Sehemu ya karibu zaidi ya Urusi bara ni umbali wa kilomita 750, umbali na Novaya Zemlya ni 370 km.

Sehemu ya kaskazini kabisa ya visiwa iko kwenye umbali wa kilomita 900 pekee kutoka ncha ya kaskazini kwa hiyo ni karibu pia na Greenland na Kisiwa cha Ellesmere cha Kanada.

Visiwa hivi 191 vina eneo kwa jumla la kilomita za mraba 16,134 na vinasambaa katika eneo lenye upana wa kilomita 375 kutoka Mashariki kwenda Magharibi na kilomita 234 kwa kutazama kusini - kaskazini.

Mwaka 2007 kulikuwa na wakazi 9 pekee, wanne wao wako kwenye kituo cha jiografia cha Kisiwa cha Hayes na watu watano wanaoangalia hali ya hewa kwenye kituo cha Nagurskoye kwenye kisiwa cha Alexandra.

Kujisomea

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Wikivoyage-Logo-v3-icon.svg Funguvisiwa ya Franz Josef travel guide kutoka Wikisafiri

  • Julius Payer: New Lands within the Arctic Circle. Narrative of the Discoveries of the Austrian Ship Tegetthoff in the Years 1872-74 (D. Appleton, New York 1877)
  • Fridtjof Nansen: Farthest North. Being the Record of a Voyage of Exploration of the Ship FRAM 1893-96. (Archilbald Constable and Co, Westminster 1897)
  • Frederick G. Jackson: A Thousand Days in the Arctic (Harper & Brothers Publishers, New York and London 1899)
  • Luigi Amedeo of Savoy: On the Polar Star in the Arctic Sea (Dodd, Mead & Co., New York 1903 and Hutchinson & Co., London 1903)
  • Anthony Fiala: Fighting the Polar Ice (Doubleday, Page & Company, New York 1906)
  • Gunnar Horn: Franz Josef Land. Natural History, Discovery, Exploration and Hunting (Skrifter om Svalbard og Ishavet No. 29. Oslo 1930)
  • Barr, Susan (1995). Franz Josef Land. Oslo: Norwegian Polar Institute. ISBN 82-7666-095-9. 
  • Lück, Michael (2008). The Encyclopedia of Tourism and Recreation in Marine Environments. CABI. ISBN 978-1-84593-350-0. 


  • viungo vya nje

Viungo vya Nje

Other Languages
Afrikaans: Franz Josef-land
azərbaycanca: Frans-İosif Torpağı
беларуская (тарашкевіца)‎: Зямля Франца-Іосіфа
Bahasa Indonesia: Daratan Franz Josef
Nederlands: Frans Jozefland
norsk nynorsk: Frans Josefs land
srpskohrvatski / српскохрватски: Zemlja Franje Josifa
Simple English: Franz Josef Land
slovenščina: Dežela Franca Jožefa
српски / srpski: Земља Фрање Јосифа
татарча/tatarça: Франц-Иосиф җире
oʻzbekcha/ўзбекча: Frans-Iosif Yeri
Tiếng Việt: Zemlya Frantsa-Iosifa