Elizabeth I wa Uingereza

Malkia Elizabeth mnamo 1585

Elizabeth I wa Uingereza (7 Septemba 1533 - 24 Machi 1603) alikuwa malkia wa Uingereza kuanzia 1558 hadi kifo chake. Alikuwa mwanamke wa tatu kutawala Uingereza kama malkia.

Aliitwa mara nyingi "malkia bikira" kwa sababu hakuolewa wala kuzaa watoto. Kutokana na neno la Kiingereza kwa bikira ("virgin") koloni la kwanza la Uingereza likaitwa "Virginia".

Wakati wake ulikuwa kipindi cha kustawi kwa utamaduni na uchumi katika Uingereza ambako William Shakespeare alitunga maigizo na tamthiliya zake, Francis Bacon aliandika falsafa yake na Francis Drake aliweka misingi ya upanuzi wa ukoloni wa Uingereza duniani. Elizabeth alihakikisha pia kipaumbele cha Kanisa Anglikana kama dini rasmi ya taifa.

Utoto

Alizaliwa katika nasaba ya Tudor kama mtoto wa mfalme Henry VIII wa Uingereza na mke wake wa pili Anne Boleyn. Hakumkumbuka mama yake aliyeuawa na mumewe akiwa mdogo wa miaka mitatu.

Alipata elimu nzuri akajua lugha sita za Kiingereza, Kifaransa, Kiitalia, Kihispania, Kigiriki na Kilatini.

Kwa miaka mingi hali ya cheo chake ilikuwa mashakani. Babake Henry VIII hakumtaka kama mrithi baada ya kumchukia mamake aliyemwua. Lakini mke wa mwisho wa Henry VIII alimshawishi mfalme kuwaingiza mabinti zake katika orodha ya ufuatano wa warithi wa cheo chake lililothibitishwa na bunge.

Other Languages
Alemannisch: Elisabeth I.
አማርኛ: 1 ኤልሳበጥ
azərbaycanca: I Elizabet
башҡортса: Елизавета I
žemaitėška: Elžbieta I
беларуская: Лізавета I
беларуская (тарашкевіца)‎: Лізавета I
български: Елизабет I
нохчийн: Елизавета I
čeština: Alžběta I.
Чӑвашла: Елизавета I
Deutsch: Elisabeth I.
suomi: Elisabet I
hrvatski: Elizabeta I.
Հայերեն: Եղիսաբեթ I
Bahasa Indonesia: Elizabeth I dari Inggris
íslenska: Elísabet 1.
ქართული: ელისაბედ I
қазақша: I Елизавета
Lëtzebuergesch: Elizabeth I. vun England
Lingua Franca Nova: Elizabeth 1
lietuvių: Elžbieta I
latviešu: Elizabete I
Baso Minangkabau: Elizabeth I dari Inggirih
македонски: Елизабета I
മലയാളം: എലിസബത്ത് I
монгол: I Элизабет
Plattdüütsch: Elisabeth I. (Tudor)
norsk nynorsk: Elisabeth I av England
Livvinkarjala: Elisabeth I
پنجابی: الزبتھ I
Runa Simi: Elisabeth I
русский: Елизавета I
संस्कृतम्: एलिजबेथ् प्रथमा
srpskohrvatski / српскохрватски: Elizabeta I
Simple English: Elizabeth I of England
slovenščina: Elizabeta I. Angleška
српски / srpski: Елизабета I Тјудор
Türkçe: I. Elizabeth
татарча/tatarça: Yelizaveta I patşabikä
українська: Єлизавета I
vepsän kel’: Elizavet I
Tiếng Việt: Elizabeth I của Anh
Vahcuengh: Elizabeth I
Bân-lâm-gú: Elizabeth 1-sè