Danna Garcia

Danna Garcia
Danna Garcia.
Danna Garcia.
Jina la kuzaliwaDanna Garcia
Alizaliwa4 Februari 1978
Kolombia
Kazi yake Mwigizaji, Mwanamuziki
Tovuti Rasmi Danna Garcia.com

Danna Garcia (amezaliwa tar. 4 Februari 1978 mjini Bogotá, Colombia) ni mwigizaji wa tamthilia, filamu na pia mwimbaji.

Ni binti wa mwimbaji muziki wa kikolombia Claudia Osuna. Danna ameanza shughuli za muziki na uigizaji toka akiwa na umri wa miaka minne.Mnamo mwaka 1994, akiwa na dada yake Claudia, waliunda bendi ya muziki, iitwayo "Café Moreno. Katika kipindi cha mwaka mmoja, waliweza kurekodi platini tatu mfululizo, na wakafanikiwa kutoa albamu iliyokwenda kwa jina la Momposino.

Mwaka huo huo Dana akaoneka kwenye ya tamthilia moja ya nchini Colombia iliyokuwa inaitwa "Café con aroma de mujer".Mnamo mwaka 1996, akawa mwigizaji bora wa kike nchini Colombia na pia nyota katika telenovela za kimexiko.

Danna Garcia pia alicheza tamthilia nyingine nyingi tu, ikiwemo ile ya Pasión de gavilanes (2003) na La Revancha (2000) hizi zilimpa sifa sana mwanadada huyu.

Filamu na Tamthilia Alizocheza

 • La Traición (2007)
 • Corazón partido (2005) .... Aura Echarri
 • Te Voy a Enseñar a Querer (2004-2005) .... Diana Rivera
 • Pasión de gavilanes (2003) .... Norma Elizondo Acevedo de Escandón
 • "Revancha, La" (2000) .... Mariana Ruiz
 • "Háblame de amor" (1999) .... Jimena
 • "Perro amor" (1998) .... Sofía Santana
 • "Al norte del corazón" (1996) .... Eloísa (1996)
 • Día es hoy, El (1996)
 • "Victoria" (1995) .... Victoria
 • Café con aroma de mujer (1994) .... Marcela Vallejo Cortez
 • "Imaginate" (1987)
Other Languages
العربية: دانا غارسيا
azərbaycanca: Danna Qarsiya
български: Дана Гарсия
Deutsch: Danna García
Ελληνικά: Ντάνα Γκαρσία
English: Danna García
español: Danna García
français: Danna García
Kreyòl ayisyen: Danna García
հայերեն: Դաննա Գարսիա
português: Danna García
română: Danna García
русский: Гарсия, Данна
srpskohrvatski / српскохрватски: Danna García
slovenčina: Danna García
српски / srpski: Дана Гарсија
Türkçe: Danna García