Bosnia na Herzegovina

Bosna i Hercegovina
Босна и Херцеговина

Bosnia na Herzegovina
Bendera ya Bosnia na HerzegovinaNembo ya Bosnia na Herzegovina
BenderaNembo
Kaulimbiu ya taifa: --
Wimbo wa taifa: "Intermeco"
Lokeshen ya Bosnia na Herzegovina
Mji mkuu43°52′ N 18°25′ E
Mji mkubwa nchiniSarajevo
Lugha rasmiKibosnia, Kikroatia, Kiserbia
Serikali
Marais

Mwenyekiti wa
halmashauri ya mawaziri
Jamhuri
Bakir Izetbegović1 (Mbosnia)
Nebojša Radmanović (Mserbia)
Željko Komšić (Mkroatia)
Nikola Špirić
Uhuru
Ilitambuliwa

6 Aprili 1992
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
51,197 km² (128)
--
Idadi ya watu
 - Julai 2006 kadirio
 - 2014 sensa
 - Msongamano wa watu
 
4,498,9762 (ya 1273)
3,871,643[1]
76/km² (ya 1163)
FedhaConvertible mark
pamoja na Euro (BAM4)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD.ba
Kodi ya simu+387

-

1 Maraisi watatu wanaobadilishanan
2 Kadirio ya CIA World Factbook [2].Bosnia na Herzegovina (Bosna i Hercegovina au Босна и Херцеговина) ni nchi ya Ulaya kusini mashariki kwenye rasi ya Balkani. Mara nyingi huitwa kwa kifupi "Bosnia" tu na watu wake "Wabosnia". Ilikuwa sehemu ya Yugoslavia hadi mwaka 1992.

Eneo lake ni km² 51,129 linalokaliwa na wakazi karibu milioni nne.

Mji mkuu ni Sarayevo.

Kati ya wakazi kuna vikundi vitatu vinavyotofautiana kiutamaduni na kidini: Wabosnia (48%), Waserbia (37.1%) na Wakroatia (14.3%). Wanadai ya kwamba lugha zao ni tofauti, lakini hali halisi ni lugha ileile ya Kislavoni. Wakati wa Yugoslavia iliitwa "Kiserbokroatia". Tofauti ziko kwa sababu Wabosnia hutazamiwa kuwa Waislamu, Waserbia kuwa Waorthodoksi na Wakroatia kuwa Wakristo Wakatoliki.

Nchi ina vitengo viwili: Shirikisho la Bosnia na Herzegovina linalounganisha maeneo ya Waislamu na ya Wakatoliki na Republika Srpska au eneo la Waserbia Waorthodoksi.

Ramani ya Bosnia na Herzegovina

Historia

Bosnia ilitokea kama eneo la pekee wakati wa Karne za kati chini ya utawala wa Dola la Uturuki.

Jina la Bosnia limetokana na mto Bosna. Jina la Herzegovina lilitokana na watemi wa kusini katika eneo la mji wa Mostar waliotumia cheo cha Kijerumani cha "Herzog" na eneo lao liliitwa "nchi ya Herzog" au "Herzegovina".

Utawala wa Kiislamu ulisababisha kugeuka kwa sehemu kubwa ya wakazi kuwa Waislamu walioendelea kutumia lugha yao ya Kislavoni.

Wakati wa kudhoofika kwa Dola la Uturuki katika karne ya 19 utawala wa nchi ulifika mikononi mwa Austria-Hungaria.

Vita kuu ya kwanza ya dunia ilisababishwa mjini Sarayevo kutokana na ma uaji ya mfalme mteule wa Austria na mke wake.

Kati ya 1918 na 1992 Bosnia na Herzegovina ilikuwa jimbo la Yugoslavia.

Baada ya uhuru ilitokea vita kali kwa sababu sehemu ya Waserbia na ya Wakroatia walitaka kuunganisha nchi au sehemu zake na Serbia au Kroatia. Wakazi wengi walifukuzwa nyumbani kwao kufuatana na maeneo ambako wanamigambo wa Waserbia au Wakroatia walitawala kufukuza wote wengine.

Jumuiya ya kimataifa iliingilia kati na kuwalazimisha washiriki kukubali amani katika mkataba wa Dayton wa 1995.

Mamlaka kuu haimo mikononi mwa serikali ya wenyeji bali mikononi mwa Kamishna Mkuu kwa Bosnia na Herzegovina anayeteuliwa na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya. Ana mamlaka ya kubatilisha sheria zilizoamuliwa na bunge, pia kuachisha mawaziri kazi.

Other Languages
беларуская (тарашкевіца)‎: Босьнія і Герцагавіна
বিষ্ণুপ্রিয়া মণিপুরী: বসনিয়া বারো হার্জেগোভিনা
Chavacano de Zamboanga: Bosnia y Hercegovina
Mìng-dĕ̤ng-ngṳ̄: Bosnia gâe̤ng Herzegovina
qırımtatarca: Bosna ve Hersek
словѣньскъ / ⰔⰎⰑⰂⰡⰐⰠⰔⰍⰟ: Босна
estremeñu: Bósnia Ercegovina
Frysk: Bosnje
गोंयची कोंकणी / Gõychi Konknni: बॉस्निया आणि हर्झगोव्हिना
客家語/Hak-kâ-ngî: Bosnia lâu Herzegovina
hornjoserbsce: Bosniska a Hercegowina
Kreyòl ayisyen: Bosni ak Erzegovin
Bahasa Indonesia: Bosnia dan Herzegovina
Kongo: Bosna
kalaallisut: Bosnia-Hercegovina
къарачай-малкъар: Босния бла Герцеговина
Lëtzebuergesch: Bosnien an Herzegowina
Lingua Franca Nova: Bosnia e Hersegovina
لۊری شومالی: بوسنی و ھئرزئگوڤین
Basa Banyumasan: Bosnia-Herzegovina
Bahasa Melayu: Bosnia dan Herzegovina
Dorerin Naoero: Boteniya me Erdegobina
Napulitano: Bosnia-Erzegovina
Plattdüütsch: Bosnien-Herzegowina
Nedersaksies: Bosnië-Herzegovina
norsk nynorsk: Bosnia-Hercegovina
Livvinkarjala: Bosnii-Hertsegovinu
Papiamentu: Bosnia Herzogovina
Norfuk / Pitkern: Bosnya a' Hersegowina
tarandíne: Bosnie-Erzegovine
संस्कृतम्: बास्निया
davvisámegiella: Bosnia ja Hercegovina
srpskohrvatski / српскохрватски: Bosna i Hercegovina
Simple English: Bosnia and Herzegovina
slovenčina: Bosna a Hercegovina
slovenščina: Bosna in Hercegovina
Gagana Samoa: Bosnia ma Herzegovina
Soomaaliga: Bosniya
Sranantongo: Bosnikondre
Türkçe: Bosna-Hersek
ئۇيغۇرچە / Uyghurche: بوسنىيە ۋە ھېرسېگوۋىنا
oʻzbekcha/ўзбекча: Bosniya va Gersegovina
vepsän kel’: Bosnii da Gercegovin
Tiếng Việt: Bosna và Hercegovina
walon: Bosneye
Wolof: Bosni
吴语: 波黑
Bân-lâm-gú: Bosnia kap Herzegovina
粵語: 波斯尼亞