Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

UN security council 2005.jpg

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ni mkono muhimu na wenye nguvu wa Umoja wa Mataifa. Baraza la Usalama linajadili masuala ya usalama na amani kati ya mataifa na kuwa na madaraka ya kutoa maazimio.

Baraza la Usalama lilikuwa na mkutano wake wa kwanza tarehe 17 Januari mwaka 1946 katika jumba la Church House mjini London. Tangu mkutano huo, baraza hilo ambalo halifungi mikutano yake, limesafiri kwa upana, likifanya mikutano katika miji mingi, kama vile Paris na Addis Ababa, ila kwa kawaida katika makao yake makuu katika jumba la Umoja wa Mataifa mjini New York.

Wanachama

Kuna wanachama 15 wa Baraza la Usalama. Kati ya hao watano ni wanachama wa kudumu na 10 ni wanachama wa kuchaguliwa ambao si wa kudumu wenye vipindi vya miaka miwili.

Mpangilio msingi umeelezwa katika Sura ya V ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Ni lazima wajumbe wa Baraza la Usalama wawe daima katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York ili Baraza la Usalama liweze kukutana wakati wowote. Jambo hili la Mkataba wa Umoja wa Mataifa limepangwa kwa makusudi kwa sababu Shirikisho la Mataifa lilishindwa mara nyingi kutatua shida za dharura.

Wanachama 5 wa kudumu ni:

Nafasi 10 zinashikwa na wanachama wa muda kwa vipindi vya miaka 2. Hao wanateuliwa na Mkutano Mkuu wa UM kulingana na kanda za UM.

Mwenyekiti wa baraza anabadilika kila mwezi kati ya wanachama.

Mwaka 2011 wanachama wa muda ni:

Other Languages
беларуская: Савет Бяспекі ААН
беларуская (тарашкевіца)‎: Рада Бясьпекі ААН
føroyskt: Trygdarráð ST
مازِرونی: امنیت شورا
norsk nynorsk: Tryggingsrådet i SN
پنجابی: بچاؤ پریہا
srpskohrvatski / српскохрватски: Savet bezbednosti Ujedinjenih nacija
slovenščina: Varnostni svet ZN
татарча/tatarça: БМО Иминлек Шурасы
українська: Рада Безпеки ООН
Bân-lâm-gú: An-chôan Lí-sū-hōe